Suruali Imeniaibisha Kwenye Daladala.....!!

Katavi

Platinum Member
Joined
Aug 31, 2009
Posts
42,023
Reaction score
12,811
Leo asubuhi nawahi zangu kwenye majukumu ya kila siku nimekumbwa na balaa.
Nilipokuwa napanda katika daladala ghafla suruali ikaachia(ikatatuka) kuanzia usawa wa maungio ya miguu mpaka usawa zip inapoanzia. Mbaya zaidi nilikuwa nimechomekea, sikushuka hadi kituo cha mwisho konda aliponiazima sare yake nikavaa kwa muda wakati fundi akinirekebishia hii iliyotatuka
Hata ofisini sikuenda tena.....
 
Duh.....Best Katavi pole sana bhana, sijui mizigo ilikuwaje huko hiyo ni siri yako.
 
kwa nini ulivaa sarawili inayokubana... Katavi...
 
Last edited by a moderator:
pole sana mkuu i think utatafuta zinazobana lakini ambazo sio tyt saana
 
pole sana ila umenifurahisha aisee sipati picha duuh
 
Katavi isiwe una swaga za wazee flani kuvaa mayeno halafu mzigo unaonekana kabisa umening'inia upande mmoja
 
kwisha habari yako Katavi...ukamwaga razi bo!
 
Last edited by a moderator:

Loh?
Pole sana Katavi, napata picha jinsi ulivyokuwa unatembea kama unashoot video ya Hakunaga..
Bwahahahahaha....
 
Last edited by a moderator:
Dah! hii kitu inaboa sana aisee, kuna siku nilikuwa ukweni, sasa katika kujifanya kuwaimpress wakwe nikajifanya nimesomea karate, kumbe bamkwe na yeye alipitia hako kakozi lakini ananichora tu. Mara akaniambia nipige side kick aone, mzembe ile kuruka nikafyetuka na suruali ikakwapuka na mbaya zaidi nikateguka shingo. Yule mamkwe ili kunipa moyo nisijiskie nishai akajidai, "Kumbe tukivamiwa na wizi tukupigie simu wewe tu bamkwe wala hatuna haja ya kuwahi polisi".
 
Hahaha hizi suruali siku hizi mimi nikinunua nampelekea fundi akazungushe uzi kwanza.

Juzi swahiba wangu alipatikana na mkasa kama wako, bahati nzuri alikuwa ofisini kwake ikabidi afunge mlango akavua suruali akaibana na Stepler akadumu nayo hadi jioni.
 
ungevaa jinsi bhana halafu upige hung hang
 
Pole mkuu Katavi ...

Ni mara chache wanaume wanadhalilika ghafla namna hizo.. Sana sana labda nauli ipotee au kubaki kwenye suruali ya jana... Ila kutatukiwa au ... Mara chache kiukweli..
 
Last edited by a moderator:
pole Katavi,juzi juzi tu hapa wadada wamekukalia kooni kwa kuwaomba chungwa leo tena suruali
 
Last edited by a moderator:

Mkuu ushuzi haukutoka kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…