Suruali za Jeans: Kwanini Nyaraka za Serikali Zinaita ni Mavazi Yasiyofaa

Suruali za Jeans: Kwanini Nyaraka za Serikali Zinaita ni Mavazi Yasiyofaa

JembeNaNyundo

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2016
Posts
533
Reaction score
652
Nimekuwa natatizwa sana na nyaraka za serikali kuhusiana na mavazi, hususani Waraka wa Utumishi Na. 1 wa mwaka 1971 unaohusu mavazi ambao ulitokana na mwongozo uliotolewa na Chama cha TANU kuhusu mavazi na pia waraka wa Utumishi wa Umma namba 3 wa mwaka 2007 kuhusu mavazi kwa watumishi wa umma ambao ulikuwa na maboresho madogo. Moja ya nguo ambayo sielewi ni kwanini inakatazwa ni suruali za jeans.

Ninajiuliza kuna sababu yoyote ya kukataza suruali ya jeans kuvaliwa kazini? Au ndio copy and paste?
 
Hakuna uhusiano wowote kati ya utendaji kazi na vazi la jinsi,huo waraka ulitakiwa ufanyiwe maboresho
 
suruali za Jeans zimeruhusiwa kuvaliwa maofisini lakini wakati wa shughuli maalum/
bado si vazi la heshima, iko siku wataonesha maungo yote (jeans tight, jeans mbenuo kata K)
Bora yapigwe marufuku tu kama huko Vyuoni. maana ilikuwa balaa
upload_2017-10-4_19-16-34.png
 

Attachments

Afadhali wangezuia wafanyakazi wao, idara nyingine hata ukienda kufuata huduma ukivaa jeans unazuiwa! Ushamba mzigo.
 
Sioni mantiki ya kumzuia mwanaume kuvaa nguo ya jeans. Hata avae jeans kama anachapa kazi, mwache avae tu.
 
kumbe hata t shirts ni marufuku!? NAKERWA NA WALIMU WANAOVAA T-SHIRTS KAMA
NDIO VAZI RASMI SHULENI
 
Back
Top Bottom