Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Unamuona huyu mdada pichani? Hana furaha. Uwanja mzima unashangilia goal matata la Ronaldo ila yeye hana amani.
Mwaka 1998, Timu ya taifa ya Brazil ilielekea Ufaransa kucheza michuano ya kombe la Dunia. Kila mmoja uwanjani alikuwa akifurahia soka safi la Kibrazil lililokuwa la nguvu na vipaji maridhawa.
Baadaye kamera za runinga ambazo zilikuwa zinaonesha mchezo huu, zikanasa picha ya mwanamke huyu wa Kibrazil mwenye sura ya kizungu na shepu ya kutokea Latini.
Baadaye ikagundulika kwamba mwanamke huyu anaitwa Susana, demu wa Supstaa wa Kibrazil Ronaldo de Lima.
Mwanamke huyu hadi leo anahesabiwa kama shetani mbele ya Wabrazil. Wanamlaani na hawataki hata kumuona. Wanaamini alifanya wakose kombe la Dunia na alikaribia kabisa kumuua nyota wao, Ronaldo de Lima.
Siku moja Ronaldo alifunga goal na akaenda kushangilia kwenye jukwaa moja hivi. Alipoangalia vizuri akaona mpenzi wake huyu amekaa na jamaa mmoja. Ronaldo akakasirika sana, kwasababu sura ya jamaa huyo haikuwa ngeni machoni pake. Kuanzia hapo akaanza kupata wasiwasi kwamba mpenzi wake anamsaliti.
Bwana Roberto Carlos, ambaye alikuwa rafiki wa Ronaldo na walikuwa wanalala chumba kimoja wakiwa kambini anasema, jamaa aliyekaa na Susana ni mtangazaji maarufu wa TV ya Brazil kwa wakati huo. Alionekana akiwa karibu na Susana baada ya kuona Ronaldo yupo kwenye timu ya Taifa.
Kesho ni fainali ya kombe la Dunia kati ya Brazil dhidi ya wenyeji Ufaransa. Usiku huu Ronaldo anapata taarifa kuwa jamaa aliyekaa karibu na Susana siku ile ndo mpemzi mpya wa Susana na wamesafiri wote kuja Ufaransa kutazama kombe la Dunia. Na wamefikia hotel moja.
Hapohapo Ronaldo anachukua simu na kumpigia Susana. Susana anakana tuhuma zote. Susana anaapa kwamba hawezi kumsaliti Ronaldo na anasema mtu yule ni rafiki tu ambaye anamfariji wakati huu ambao yeye hayupo.
Ronaldo haamini. Carlos anasema;
"Ronaldo akakata simu kwa hasira na akaanza kulia kwa muda mrefu hadi usingizi ulipomkuta akiwa kwenye msongo wa mawazo. (Kumbuka kesho ndo fainali na Ronaldo ni mashine ya kutegemewa na wabrazil wote.)
Asubuhi nilipoamka nikakuta Ronaldo anakoroma kama mtu anayekaribia kukata roho. Kumbe alikuwa anakaribia kuumeza ulimi wake.
Ilikuwa vilevile kama ambavyo yule muigizaji wa kike Marilyn Monroe alipofariki kwa kuumeza ulimi wake.
Haraka madaktari walifika na kumhudumia. Aliporejewa na fahamu akakuta muda umesogea sana na bado saa chache fainali ipigwe. Wachezaji wengine walikuwa wanapewa maelekezo ya mwisho.ili wakapashe misuli.
Kila mchezaji alikuwa anawaza hali ya Ronaldo na vipi wangeikabili Ufaransa bila chuma chao cha magoli.
Ronaldo akakimbia moja kwa moja hadi kwa kocha na akamwambia, "Zagallo, nataka nicheze mechi hii." Kocha akakataa kwa madai kwamba bado hayupo sawa kisaikolojia na ulimi haujaimalika, pia madaktari wakashauri asicheze kwani akili zake hazipo sawa.
"Msiniambie hivyo, najijua mwenyewe, Najiona nipo vizuri na ninaweza kucheza. Na nitacheza, Zagallo naomba usinizuie.''
Kila mmoja akamshangaa Ronaldo. Alikuwa hovyo na timu nzima ikahudhunika.
Saa 1:38 jioni, Zagallo akapeleka line up kwa kamisaa wa FIFA huku jina la Ronaldo likiwa halipo na nafasi yake akapangwa Edmundo. Brazil wakapigwa 0-3.
Ufaransa wakachukua kombe. Ronaldo akampoteza Susana milele. Wabrazil wakaahidi kumuua Susana akionekana popote, wanaamini kama siyo Susana basi Ronaldo angefanya maajabu siku ya fainali.
Mwanaume kupoteza kwenye mapenzi hakujaanza juzi.