Suti aina ya Zoot kama anavyoielezea Malcom X

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Kwenye biography yake, Malcom X anaelezea jinsi alivyonunua suti aina ya zoot alivyofika jijini Boston.

Suruali ya bluu, magotini ikiwa na upana wa nchi thelathini, kisha inapungua upana kuelekea chini hadi kufikia upana wa nchi kumi na mbili kwenye pindo la chini. Koti lake lilikuwa refu, lilinibana kiunoni na kujiachia kuanzia magotini.

Muuzaji aliniambia kuwa watanipatia na mkanda mwembamba wa ngozi wenye herufi “L”—kifupisho cha jina langu kama zawadi. Aliniambia kuwa natakiwa kununua na kofia pia, nilifanya hivyo, nilinunua kofia ya bluu iliyokuwa na unyonya mrefu pembeni. Kisha nikapewa zawadi nyingine, myororo mrefu wenye rangi ya dhahabu ambao niliuning’iniza kwenye luksi.

Kwenye movie ya Malcom X aliyocheza Denzel Washington hivi ndivyo alivyoonekana.

3d6046336655600c34f6aeaa71e34a4e.jpg
 
Lyc...

Nina kumbukumbu nyingi za Malcolm X kutoka udogoni na baadae mtu mzima na nilikopita.

Movie ya Malcolm X niliitazama nikiwa mji mdogo Uingereza wakati huo mimi kijana.

Kisha kwengine duniani nimekutana za kumbukumbu ya Malcolm X.

Nimefika 125th Street Harlem, New York na ninayo picha.

Hii ilikuwa mitaa yake Malcolm.
Nmeuna pia ukumbi aliouliwa Malcolm X

Nilipokuwa New York ndiyo biography yake mpya ilikuwa imetoka iliyoandikwa na Manning Marable, "A Life of Reinvention."

Wasifu wake wa kwanza ulioandikwa na Alex Haley, "The Autography of Malcolm X," (1965)inasemekana, Haley alibadilisha baadhi ya mambo baada ya kifo cha Malcolm X.

Malcolm X mimi alikuwa "hero," wangu na nilisoma wasifu wake ule wa Haley labda nina miaka 15.

Spike Lee katufanyia hisani kubwa kwa kutengeneza "movie,"ya Malcolm X, "Malcolm," na kumtia Dezil Washington kama Malcolm.

Kwangu mimi Malcolm X na nyakati zile zinanikumbusha mengi, muziki wa Sam Cooke, "Twist in the Night Away," Nat King Cole, "Ramblin' Rose," Cassius Clay na Sony Liston, kabla hajawa Muhammad Ali.

Hizi zilikuwa nyakati za utoto wangu nikikua Dar es Salaam nikisikiza muziki wa Chipukizi wa akina Hussein Shebe, Henin Seif, Raymond Chihota, Cuthbert Sabuni na The Blue Diamonds na alikuwapo mtu wetu wenyewe Sal Davis...miaka imeruka na ujana umetoweka kama moshi.

Katika maisha ya Malcolm X jinsi yalivyobadilika yanaendana na maisha ya wengi tulioishi miaka ile "The Roaring 60s," na kwa hili tumshukuru Allah kwa kutuongoza.
 
Lyc...
Nina kumbukumbu nyingi za Malcolm X kutoka udogoni na baadae mtu mzima na nilikopita.

Movie ya Malcolm X niliitazama nikiwa mji mdogo Uingereza wakati huo mimi kijana.

Kisha kwengine duniani nimekutana na kumbukumbu ya Malcolm X.

Nimefika 125th Street Harlem, New York na ninayo picha.

Hii ilikuwa mitaa yake Malcolm.

Nilipokuwa New York ndiyo biography yake mpya ilikuwa imetoka iliyoandikwa na Manning Marable, "A Life of Reinvention."

Wasifu wake wa kwanza ulioandikwa na Alex Haley, "The Autography of Malcolm X," (1965)inasemekana, Haley alibadilisha baadhi ya mambo baada ya kifo cha Malcolm X.

Malcolm X mimi alikuwa "hero," wangu na nilisoma wasifu wake ule wa Haley labda nina miaka 15.

Spike Lee katufanyia hisani kubwa kwq kutengeneza "movie,"ya Malcolm X, "Malcolm," na kumtia Dezil Washington kama Malcolm.

Ahsante kwa historia hii. Niliipenda sana Movie yake. Sasa ndiyo nasoma wasifu wake alioandika Alex Haley. Niliona uchambuzi wanasema alibadilisha mengi na mengine alimshauri kabla hajafa yasiwekwe. Ni mtu wa aina yake sana.
 
Kutoka kuwa jambazi wa kutumia bastola hadi kiongozi wa umma wa Waislam Weusi Marekani.
 
Lyc...
Nina kumbukumbu nyingi za Malcolm X kutoka udogoni na baadae mtu mzima na nilikopita.

Movie ya Malcolm X niliitazama nikiwa mji mdogo Uingereza wakati huo mimi kijana.

Kisha kwengine duniani nimekutana za kumbukumbu ya Malcolm X.

Nimefika 125th Street Harlem, New York na ninayo picha.

Hii ilikuwa mitaa yake Malcolm.
Nmeuna pia ukumbi aliouliwa Malcolm X

Nilipokuwa New York ndiyo biography yake mpya ilikuwa imetoka iliyoandikwa na Manning Marable, "A Life of Reinvention."

Wasifu wake wa kwanza ulioandikwa na Alex Haley, "The Autography of Malcolm X," (1965)inasemekana, Haley alibadilisha baadhi ya mambo baada ya kifo cha Malcolm X.

Malcolm X mimi alikuwa "hero," wangu na nilisoma wasifu wake ule wa Haley labda nina miaka 15.

Spike Lee katufanyia hisani kubwa kwq kutengeneza "movie,"ya Malcolm X, "Malcolm," na kumtia Dezil Washington kama Malcolm.

Kwangu mimi Malcolm X na nyakati zile zinanikumbusha mengi, muziki wa Sam Cooke, "Twist in the Night Away," Nat King Cole, "Ramblin' Rose," Cassius Clay na Sony Liston, kabla hajawa Muhammad Ali.

Hizi zilikuwa nyakati za utoto wangu nikikua Dar es Salaam nikisikiza muziki wa Chipukizi wa akina Hussein Shebe, Henin Seif, Raymond Chihota, Cuthbert Sabuni na The Blue Diamonds na alikuwapo mtu wetu wenyewe Sal Davis...miaka imeruka na ujana umetoweka kama moshi.

Katika maisha ya Malcolm X jinsi yalivyobadilika yanaendana na maisha ya wengi tulioishi miaka ile "The Roaring 60s," na kwa hili tumshukuru Allah kwa kutuongoza.
Malcom X a muslim akazikwa kikristo kwa nini tuelezee hapa Mohamed Said
 
Alizikwa kwenye makaburi ya kanisa na maiti yake iliwekwa kwenye jeneza kama la wakristo na ikaagwa na umati wa watu ikiwa wazi kabisa

Mdukuzi,
Swali lako nitalijibu kwa kirefu kidogo.

Kuna mambo katika maisha yangu hata mimi hunistaajabisha jinsi Allah alivyoweza kuniunganisha na watu na nchi ambazo mimi nitakuja baadae kuwafunza wengine.

Naamini unesoma jinsi mimi katika utoto wangu nilivyokuwa ''connected' na Malcolm X na Muhammad Ali na nikafika nchi na sehemu ambazo watu hawa walitengezeza historia zao mimi sasa nikiwa mtu mzima.

Malcom X unaweza kusema fikra na mtazamo wake kuhusu suala la rangi na ubaguzi zilibadilika baada ya kukutana na Msudani mmoja jina lake Ahmed Osman.

Huyu ndiye aliyemfahamisha Malcolm X kuwa Uislam hauruhusu ubaguzi wa iana yeyote na yeye kuwaita Marekani Weupe mashetani si sawa.

Kisa kirefu.
Huu ndiyo ukawa mwanzo wa urafiki wa Malcolm X na Osman.

Malcolm X kupitia Osman aliweza kwenda hadi Sudan na akazungumza University of Khartoum na akafika hadi Omdurman.

Omdurman kuna historia kubwa sana ya Mahdi aliyepigana vita na Waingereza kukomboa Sudan.

Safari hii ilimfungua macho Malcolm kuwaona Waislam kwa karibu.

Nimebahatika kufika University of Khartoum na Omdurman ambao ni mji karibu sana na Khartoum.

Sijapata kuona duniani kokote miji mikubwa miwili iliyo karibu kwa kiasi hicho.
Mfano Moshi na Arusha iwe ilipo Kiborloni kwa wanaoijua miji hii miwili.

Baada ya safari hii ya Sudan na baada ya Malcolm X kujitoka katika Nation of Islam Malcom akatoa shahada na kuwa Orthodox Muslim yaani huu Uislam unaofahamika si Black Muslim.

Malcolm akaenda Hijja na huko ndiko imani yake ilipokaa sawasawa.

Maziko yake New York yaligubikwa na kampeni chafu ya kuzuia watu maarufu kuhudhuria.

Kama usemavyo pale Harlem Malcolm anaonekana katika sanduku na watu wakimuaga.

Kitu ambacho hakikuonyeshwa ni kuwa baada ya pale maiti yake ilitolewa katika sanduku na akazikwa kwa taratibu za Kiislam.

Kaburi lilichimbwa na Waislam na sala ya jeneza ikafanyika kama sheria inavyoelekeza.

Aliyeongoza haya yote alikuwa Ahmed Osman.
 
Mdukuzi,
Swali lako nitalijibu kwa kirefu kidogo.

Kuna mambo katika maisha yangu hata mimi hunistaajabisha jinsi Allah alivyoweza alcolmkuniunganisha na watu na nchi ambazo mimi nitakuja baadae kuwafunza wengine.

Naamini unesoma jinsi mimi katika utoto wangu nilivyokuwa ''connected' na Malcolm X na Muhammad Ali na nikafika sehemu ambazo watu hawa walipotengezeza historia zao mimi sasa nikiwa mtu mzima.

Malcom X unaweza kusema fikra na mtazamo wake kuhusu suala la rangi na ubaguzi zilibadilika baada ya kukutana na Msudani mmoja ina lake Ahmed Osman.

Huyu ndiye aliyemfahamisha Malcolm X kuwa Uislam hauruhusu ubaguzi wa iana yeyote na yeye kuwaita Wmarekani Weupe mashetani si sawa.

Kisa kirefu.
Huu ndiyo ukawa mwanzo wa urafiki wa Malcolm X na Osman.

Malcolm X kupitia Osman aliweza kwenda hadi Sudan na akazungumza University of Khartoum na akafika hadi Omdurman.

Safari hii ilimfungua macho Malcolm kuwaona Waislam kwa karibu.

Nimebahatika kufika University of Khartoum na Omdurman ambao ni mji karibu sana na Khartoum.

Sijapat akuona duniani kokote miji mikubwa miwili iliyo karibu kwa kiasi hicho.
Mfano Moshi na Arusha iwe ilipo Kiborloni kwa wanaoijua miji hii miwili.

Baada ya safari hii ya Sudan na baada ya Malcolm X kujitoka katika Natioin of Islam Malcom akatoa shahada na kuwa Orthodox Muslim yaani huu Uislam wa kweli si Black Muslim.

Malcolm akaenda Hijja na huko ndiko imani yake ilipokaa sawasawa.
Maziko yake yaligubikwa na kampeni chafu ya kuzuia watu maarufu kuhudhuria.

Kama usemavyo pale Harlem Malcolm anaonekana katika sanduku na watu wakimuaga.

Kitu ambacho hakikuonyeshwa ni kuwa baada ya pale maiti yake ilitolewa katika sanduku na akazikwa kwa taratibu za Kiislam.

Kaburi lilichimbwa na Waislam na sala ya jeneza ikafanyika kama sheria inavyoelekeza.

Aliyeongoza haya yote alikuwa Ahmed Osman.
Kumbe lakini ile kuagwa na halaiki katika open cofin ikoje hiyo katika orthodox muslim
 
Hoja yangu iko hapo ilikuwaje akaoneshwa
Mdukuzi,
Ilikuwaje ikawa vile sijui labda nitoe fikra zangu.
Uislam uliokuwapo ni wa Black Muslim.

Malcolm kawa Ordhodoc Muslim miezi michache na ndipo umauti ulipomfika.

Waliomzunguka katika watu wake wote walikuwa Black Muslim.

Hili nina hakika nalo.

Mke wa Malcolm X Betty yeye ndiye akamuomba Ahmed Osman ahakikishe kuwa mumewe anazikwa kama sharia inavyosema.

Hapo ndipo Osman alipoingia kati na kuyaweka mazishi ya Malcolm X kama sharia inavyotaka.
 
Back
Top Bottom