Suti sio vazi linalomfaa kila mtu

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2014
Posts
4,051
Reaction score
12,954
Kwenye matukio maalum watu wanpenda kupendeza, wanapenda waonekane wamependeza mara nyingi watu hupendelea kuvaa vazi la suti ili kupendezesha zaidi muonekano wao.

Lakini suti sio vazi linalimpendeza kila mtu, watu wengine wakivaa suti wanakua vituko lakini kibaya zaidi ni kuvaa suti yenye rangi mbaya na imeshonwa vibaya.

Mfano, rangi ya suti waliovaa kina Mwana FA kwenye harusi ya AY ilikua rangi mbaya sana na iliwafanya waonekane wa kawaida sana kama waimba kwaya wa Boni Mwaitege. Sijui nani aliwashauri wavae ile rangi ya kijivu angalau AY alitupia black akaonekana wa tofauti.

Lakini pia uchaguzi wa rangi kwenye matukio maalum una maana, sio kwa kua ni suti unajivalia tu kimo pia, watu warefu hupendeza zaidi kwenye suti iliyodizainiwa na kushonwa vizuri kuliko wafupi.

Ukiona unashindwa kabisa vaa rangi nyeusi au dark blue, hazijawahi kumuangusha mtu, ni rangi zisizo isha muda wake.

Vazi la suti sio la kila mtu, kama suti haikupendezi achana nayo, vaa kanzu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…