MAJIBU YA WAZIRI AWESO
Mdau; Hili ni bomba la inchi 2 na moja la robo tatu, mabomba hayo ni sehemu ya mabomba yaliyotengenezwa na Mamlaka yetu ya Maji Singida SUWASA baada ya kukatwa kwa bahati mbaya na Wakala wa Barabara TARURA walipokua wakitekeleza Majukumu yao.
Nimelifuatilia kwa undani na nimejiridhisha pasipo chembe ya shaka. Nimhakikishie Mdau kwamba tayari Maji yamedhibitiwa tangu jana mchana wa tarehe 13 Nov. 2024.