Suzuki Escudo ( 3 doors) Fuel Consumption

Kajuni

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2009
Posts
483
Reaction score
186
Jamani wanajamvi naomba kuwakilisha kilio changu cha muda mrefu kwani naamini hapa ni sehemu maalumu ya kupata msaada. Nikwamba nina gari aina ya Suzuki Escudo CC 1,500 cc ya mwaka 1997. Hii gari niliagiza moja kwa moja kutoka japani takribani miaka 4 iliyopita. Historia fupi ni kwamba siku nilipokwenda kuitoa bandarini hapo hapo nilianza kupata changamoto. Ilikuwa na miss kubwa sana. Basi haraka haraka mafundi ( vishoka) walinishauri kubadili plugs. Nikafanya hivyo kwa kuwa nilikuwa na muemuko na gari mpya. Lakini kwa bahati mbaya tatitzo halikwisha na ilipelekea niende mpaka pake karume kwani niliambiwa kuna mafundi wazuri.
Nilipofika pale mafundi walianza kazi. Cheki plugs, control box etc etc na baadae wakasema gari ina "miss dume" hizi ni teminology za mafundi kama miss ni kubwa mno. Baada ya jitiada za mda mrefu tatizo halikutatuliwa. Basi fundi mmoja alijitokeza na kusema gari inaitaji tuangalie mfumo mzima wa mafuta. So kesho yake wakashusha tanki, wakasafisha, wakabadili fuel filter, na plugs ( hapa kila mtu anasema plugs tofauti tofauti?? sie hatuna ujuzi tunasikiliza tu. Lakini miss ilikuwa pale pale. Basi wataalaum wakashauri tukate Cylinder head. Nikafanya hivyo. Hela ilikuwa sio tatizo. Tulikata Cylinder head mara mbili lakini miss bado ipo na gari ilikuwa inatetemeka ikikaa silencer. Yaani unaweza kunotice kabisa kwamba gari haiko sawa.
Baada ya jitiada kidoogoo miss iliondoka lakini fuel consumption ikawa kubwa sana yaani 1 lt kwa Km 5. Basi jopo la mafundi wakakaa na kunishauri nibadili engine kwani ilokuwepo haifai( wenyewe walisema ni toleo la Ulaya na spare parts huku hakuna so niweke Engine za huku Africa. Hakika nilichoka na nikaipumzisha gari kwa mwaka mmoja nikijipanga. Baada ya kipindi hicho nilipata hela tukabadili Engine. Chakushangaza miss iliondoka kidogo nikacheza na mafundi mbali mbali na naona kuna mabadiliko. Gari ni nyepesi na inachanganya vizuri.
Tatizo consumption ya mafuta sio nzuri ilinganishwa na size ya engine average ni 7 km kwa lt 1. Nikiuliza wenzangu wenye magari kama yangu wanasema inatakiwa angalau iwe 9 ama kumi. Swali wadau nifanye nini? Nimebadili mpaka pump ya kwenye tanki etc etc.

Tatizo jingine Usukani ni Mgumu mnoo? Nimebadili vifaa vinavyo usiana na usukani mpaka basi lakini ishu ipo pale pale.

In summary gari yangu inakula mafuta na pia usukani mgumu. Naoomba ushauri wa nifanye nini. Ningeweza kuiuza hii gari lakini nina mapenzi na Escudo 3 doors. Na pia morally sipendi kumuuizia mtu kitu ambacho naona sio kizuri kwangu. Kama ikipona basi ntaamua kuendelea kuishi nayo ama kuiuza.

Ushauri tafadhali.
 
Mkuu hilo ni gari au jini????Manake litakufilisi kaka.Cha kufanya tengeneza ikipata nafuu uza haraka.Kuna watu wao magari sumbufu ni burudani kwao
 
Mkuu hilo ni gari au jini????Manake litakufilisi kaka.Cha kufanya tengeneza ikipata nafuu uza haraka.Kuna watu wao magari sumbufu ni burudani kwao
Askante kwa ushauri nasubiri mafundi waseme wanaweza ama hawawezi
 
Angalia cable za plug mkuu na weka plug nzuri NGK ziko vizuri,kingine badili nozeli zote nne utasahau hayo matatizo ya ulaji wa mafuta na misi.sababu gari inaweza kuwa na misi kwa mbali kutokana labda cable ina leakage,
 
Yan Hii gari na manzi yangu,, gari yako yala ela zaidi..
Boss io gari kimeo me nina Suzuki Ya 1994 inaperfom vyema ,paka raha,, hio iuze
 
Mkuu ukipata solution uje tubadilishane uzoefu.mimi nna tatizo hilohilo nna mark II grand 110 la 2002.ni zito na linakula wastani wa lita 1 kwa km 5.5 pia stering yake ni ngumu
Nimebadili plugs,safisha pump kwenye tank,safisha nozel lakini wapi bado zito na linabugia wese balaa hata kama ni foleni za dar lakini hii ni zaidi.mwenye solution tujuzane tafadhali
NB sitaki kuliuza nalipenda sana kwaiyo napokea ushauri wa nini cha kufanya apart from kuliuza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…