Suzuki escudo inakula mafuta sana

Suzuki escudo inakula mafuta sana

Darvon

Member
Joined
Apr 14, 2018
Posts
93
Reaction score
74
Hii ni suzuki escudo old model 1995 mwanzo ilikuwa inakula mafuta kawaida sana ila baada ya muda ikaanza kutumia mafuta sana, yaani mafuta ya sh 5000 hayamalizi hata kilomita 10.

Kuna mtu aliniambia kuwa kuna button zinasababisha gari inywe mafuta sana ila sasa sielewi ni zipi hizo.

Wajuvi wa hili jambo ninaomba mnisaidie mawazo ni wapi ninakosea.
 
Mkuu let me share with you story yangu

Nina suzuki escudo ya 1994, niliipaki kwa mwaka mmoja mwaka jana mwishoni nkaamua kiamsha, nkaipiga service kubwa na kila kitu, ikawa ina shida ya kuchelewa kubadilisha gear, yan gari zito bila sababu, nkasafiri nalo kama km 650 Hivi kija Dar, kupima consumption ikawa 8km/l, kukaa hapo Dar na jam na ac likawa latumia 5km/l.

Nikakipeleka garage moja fundi akaniambia shida ni gear box, akataka ninune mpya kwa 1.3M nkakataaa maana na hela Ilikiwa imeisha, nkasema nianze badilisha small possible things ambazo zaweza sababisha.. nkabadilisha fuel filter, siku nimeibadilisha hali ikawa mbaya mara tatu maana na nguvu ya gari iliisha yote, hata kupata speed 40kph ikawa shida.

Then nkaenda garage moja tu randomly mitaa ya gerezani, wakanionyesha jamaa mmoja fundi, bila kumwelezea tatizo jamaa aliniuliza straight mbona watembea na gari lina miss hivyo,, akafungua bonet na akaomba spana zake mbili in less than 5mnts,, jamaa akafix kila kitu na gari ikawa na zaidi ya nguvu sanah na fuel ikawa nzuri 11.5km/l japokuwa najua inaweza kwenda zaidi yahapo kuna modifications zaidi za kufanya.

Tatizo:
Shida ilikuwa wamekosea kufanya timing wakati nabadilisha timing belt., jamaa aliset timing vizuri yakawa yameisha

Ni pm nkutumie namba za fundi kama upo Dar umpekelee atarekebisha tatizo fasta.

Swali:
Mwanzo ilikuwa inakula mafuta kwa rate gani!?
 
Mkuu let me share with you story yangu

Nina suzuki escudo ya 1994, niliipaki kwa mwaka mmoja mwaka jana mwishoni nkaamua kiamsha, nkaipiga service kubwa na kila kitu, ikawa ina shida ya kuchelewa kubadilisha gear, yan gari zito bila sababu, nkasafiri nalo kama km 650 Hivi kija Dar, kupima consumption ikawa 8km/l...
Kiongozi nami nipatie namba ya huyo fundi, maana nimechoka kwenda kwa mafundi, Rav4 yangu kama natembea na sheli kwenye gari hahaaaa...
 
Mkuu tafadhali tuwekee namba hapa na sisi tuwasiliane na fundi. Mimi nina Corolla niliweka wese/petrol 5 ltrs shekilango nikaenda airport/JNIA nikarudi Upanga/ Sea View taa inawaka (na kulikua hakuna foleni kabisa)
 
Wakuu

Salama kabisa

Magari yote mliotaja hapo yote ni ya fuel injection na ndio mtaalamu wake

Niombe swala moja

Kuweka number ya mtu public bila ruhusa yake sio ustarabu naomba mni PM ntawatumia number bia PM moja kwa moja

Shukran
 
Wakuu

Salama kabisa

Magari yote mliotaja hapo yote ni ya fuel injection na ndio mtaalamu wake...
sa siumuulize kwanza kwa kuweka namba hake hapa u.emsaidia kuongeza wateja
 
Mkuu let me share with you story yangu

Nina suzuki escudo ya 1994, niliipaki kwa mwaka mmoja mwaka jana mwishoni nkaamua kiamsha, nkaipiga service kubwa na kila kitu, ikawa ina shida ya kuchelewa kubadilisha gear, yan gari zito bila sababu, nkasafiri nalo kama km 650 Hivi kija Dar, kupima consumption ikawa 8km/l, kukaa hapo Dar na jam na ac likawa latumia 5km/l, nkakipeleka garage moja fundi akaniambia shida ni gear box, akataka ninune mpya kwa 1.3M nkakataaa maana na hela Ilikiwa imeisha, nkasema nianze badilisha small possible things ambazo zaweza sababisha.. nkabadilisha fuel filter, siku nimeibadilisha hali ikawa mbaya mara tatu maana na nguvu ya gari iliisha yote,, hata kupata speed 40kph ikawa shida,
Then nkaenda garage moja tu randomly mitaa ya gerezani, wakanionyesha jamaa mmoja fundi, bila kumwelezea tatizo jamaa aliniuliza straight mbona watembea na gari lina miss hivyo,, akafungua bonet na akaomba spana zake mbili in less than 5mnts,, jamaa akafix kila kitu na gari ikawa na zaidi ya nguvu sanah na fuel ikawa nzuri 11.5km/l japokuwa najua inaweza kwenda zaidi yahapo kuna modifications zaidi za kufanya.

Tatizo:
Shida ilikuwa wamekosea kufanya timing wakati nabadilisha timing belt., jamaa aliset timing vizuri yakawa yameisha

Ni pm nkutumie namba za fundi kama upo Dar umpekelee atarekebisha tatizo fasta

Swali:
Mwanzo ilikuwa inakula mafuta kwa rate gani!?
Nashukuru sana mkuu, japo nimechelewa kukupa feedback ni kutokana na kutokuingia kwenye mtandao.

Fuel consumption nikifanya makadirio ni 12 km per litre kipindi bado ipo sawa.

Nakupm mkuu kwa mengine zaidi.

Asante.
 
Wakuu nadhan wote namba nimewatumia PM.

Ntaomba mlete mrejesho pia baada ya kuonana na fundi tujuzane shida mbalimbali.
 
Hyo gari haiwezi kuwa na fuel conception ya hivyo hata iwe mbovu kiasi gani,mambo ya kuzingatia hakikisha hai smoke nyuma kwenye exhaust,then kama ina moshi mweusi kutakuwa engine missfuring.au tuwasiliane 0716295687.

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
kuna mambo mengi ya kuongeza unywaji wa mafuta kwenye gari bila shaka gari lako litakuwa na miss,waweza pia kutumia hii namba ipo whatsapp 0782738750.

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
Habari mkuu naomba uni pm pia namba ya Fundi wako,
 
Mkuu tafadhali tuwekee namba hapa na sisi tuwasiliane na fundi. Mimi nina Corolla niliweka wese/petrol 5 ltrs shekilango nikaenda airport/JNIA nikarudi Upanga/ Sea View taa inawaka (na kulikua hakuna foleni kabisa)

Hivi 5 ltrs taa inaweza kuzima kweli
 
Wakuu Mkitoa feedback itakuwa vyema sanah

Shurkan kwa Mdau mmoja aliona hii post nkamtumia namba za simu za fundi kanipa Mrejesho kwa PM kuwa shida zimeisha kbsah za gari lake

Tupeane mrejesho wakuu
 
Mkuu let me share with you story yangu

Nina suzuki escudo ya 1994, niliipaki kwa mwaka mmoja mwaka jana mwishoni nkaamua kiamsha, nkaipiga service kubwa na kila kitu, ikawa ina shida ya kuchelewa kubadilisha gear, yan gari zito bila sababu, nkasafiri nalo kama km 650 Hivi kija Dar, kupima consumption ikawa 8km/l, kukaa hapo Dar na jam na ac likawa latumia 5km/l, nkakipeleka garage moja fundi akaniambia shida ni gear box...

Naomba namba mkuu japo nipo arusha anisaidie mkuu
 
Wakuu Mkitoa feedback itakuwa vyema sanah

Shurkan kwa Mdau mmoja aliona hii post nkamtumia namba za simu za fundi kanipa Mrejesho kwa PM kuwa shida zimeisha kbsah za gari lake

Tupeane mrejesho wakuu
Naomba namba za huyo fundi
 
Back
Top Bottom