Suzuki Escudo. Mwenye kuijua Spea, Mafuta & Utunzaji

Wakuu katika kuzunguka mtandaoni nimepata Suzuki Escudo 2700cc, MT, japo Bei imechangamka Ila naimudu. Mwenye kujua gari tajwa anishauri kabla sijatuma pesa. Asanteni

View attachment 2118627
Mmojawapo wa SUV ngumu kwa mazingira ya kiafrika. Humo weka gunia zako za kutosha inatembea vizuri tu. Ukipata ya diesel utafurahi zaid
 
Suzuki ni gari ngumu na inamudu mazingira yote, Spea zipo za kutosha.

Kwanini umechagua yenye cc kubwa hivi! Mbn zipo nzuri za cc ndogo? Hata kama utamudu gharama za mafuta shida utapata utakapotaka kuliuza. Wabongo siku hizi wananunua magari yenye cc chini ya 1500 ndo maana unaona IST zimetapakaa.
 
Acha kupangia watu maisha. Eti ukitaka kuuza. Kakuambia ananunua ili auze? Madalali mnawaza kuuza tu (joke)
 
Aisee hizi gari ni Roho ya Paka mm toka nazaliwa naikuta nyumbani mpk hivi majuzi mzee alipoamua kuiuza na akanunua nyingine Suzuki

Usiache iyo gari tena ni Manual utatumia wewe mpk wajukuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…