Suzuki kei yangu inakosa nguvu kwenye mlima

Suzuki kei yangu inakosa nguvu kwenye mlima

Mijicho

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2009
Posts
282
Reaction score
219
Habari wadau,

Nina kagari kangu Suzuki kei CC650, pia kana turbo. Tatizo lake kubwa ni kwenye mlima kanaishiwa nguvu kabisa.

Naomba ushauri wenu kabla sijaenda kwa hawa mafundi pasua kichwa.
 
Habari wadau,

Nina kagari kangu Suzuki kei CC650, pia kana turbo. Tatizo lake kubwa ni kwenye mlima kanaishiwa nguvu kabisa.

Naomba ushauri wenu kabla sijaenda kwa hawa mafundi pasua kichwa.
Nakushauri fanya diagnosis...

Pia angalia fuel pressure regulator..huenda imechoka...

Air filter huenda imechoka sana na ni chafu

Spark plugs huenda zimechoka sana..

Vipi ulaji wa mafuta umeongezeka au upo normal..?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha utani mkuu. Toka lini hako kagari kakawa na nguvu kwenye mlima? Hako hiyo ni kawaida yake!
 
Hapo mkuu kama upo makini sana yawezekana sio mliman tuu bali hata tambarare sema hujakuwa makini kuchunguza sema ww una note zaidi mlimani.


Swali hiyo gari ni automatic au manually??.
Kama automatic basi kuna weza kukawa na shida mbili gearbox au engine performance ishakuwa sifuri..

Unaposema inakosa nguvu mlimani hata ikiwa kwenye namba 1??.inakuwa inasinzia??.yaani ukaiendesha chini ya speed 40. Au 30 inakuwaje??.
Au endesha speed isizidi 20 maana hapo unakuwa upo kwenye gear namba 1 gari inakuwaje??.
Je vip performance ya engine?? Kwenye silensa ukipiga less??.

Tufanye ishu ni kwenye engine kagua.
Petrol filter ,air clener,spark plug,
Kama petrol filter majanga basi kagua na nozel..

Mambo ni mengi jazia nyama au jibu maswali ili kujua shida iko wapi??.engine au gearbox??.
Au kama upo dar karibu sana JO AUTO TECH #0627136700#
 
LEGE,
Tuseme inavyoonekana ni kama inachelewa kubadilisha gear,na zaidi inaonekana kwenye mlima,tambarare pengine turbo inasaidia,engine inaonekana kama iko poa kwa kila anayeikagua kwa haraka haraka,ukiendesha kwa speed kali inapunguza mwendo kabisa ,labda nikiweka 2,au L naona ndio inapata nguvu,hi ni automatic
 
Wadau habari,
Gari iko sokoni hiyo Dar es Salaam
Suzuki kei milango mitatu,siti 4
Mwaka 1999
Cc 650
Bei 4M maongezi yako

Kadi original ilipotea lakini mchakato wa kupata duplicate umeshaanza.

IMG_20191230_144945.jpg
IMG_20191230_144933.jpg
IMG_20191230_144920.jpg
IMG_20191230_144907.jpg
IMG_20191230_145000.jpg
IMG_20191230_145013.jpg
 
Unauza gari afu haina kadi?!? How?!?
Ipo certified copy,kama unajua maana ya kadi ni ushahidi tu wa umiliki wa gari,lakini mtu anayehitaji gari na ana shida nayo anaweza kujiridhisha tra bila wasiwasi,akalinganisha majina gari iliyosajiliwa vs kitambulisho cha mmiliki,Na zoezi la kupata duplicate likiendelea,Asante kwa kuniomba ufafanuzi
 
Kama kadi ya gari ni ushahidi tu wa umili taasisi za fedha zisingekua zinatoa mkopo kwa kutumia kadi ya gari huku wakijua kama unaweza kusema tu kadi imepotea na ukapata nyingne

Maliza kwanza kila kitu ndio uuze hamna mtu anaetaka kununua kitu cha mashakamashaka unaharakia nn

Mijicho,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kadi ya gari ni ushahidi tu wa umili taasisi za fedha zisingekua zinatoa mkopo kwa kutumia kadi ya gari huku wakijua kama unaweza kusema tu kadi imepotea na ukapata nyingne

Maliza kwanza kila kitu ndio uuze hamna mtu anaetaka kununua kitu cha mashakamashaka unaharakia nn

Mijicho,

Sent using Jamii Forums mobile app


Hao wanaotoa mkopo kwa kutumia kadi ya gari wanakosea ,wanachotakiwa kufanya ni kuongeza imiliki wa gari kwenye system kule Tra halafu ndio wanaprint,maana ukimpa mtu kadi tu akakupa hela,then naweza bado kutengeneza ingine duplicate nikamuachia original,na gari nikauiza bado,so kinachoangaliwa ni kule TRA.Halafu naomba tusipangiane muda wa kuuza gari,kama hununui wewe watanunua wengine
 
Back
Top Bottom