Swahili makes history as first African language recognized by Twitter- Thanks Larry Madowo and Kenya at Large

Wakenya kila kitu chenu mpaka kiswahili mnasema ni chenu lakini ukitaka kujua nani mwenye kiswahili chake hupati shida ukimuweka mkenya changanya na mganda ongeza na miongo halafu muweke na mtanzania utapata jibu

Sehemu marehemu anapoitwa mwenda zake na mke kuitwa bibi unasema ndipo kilipozaliwa kiswahili hivi ni vichekesho

Hata hivyo tunashukuru kwa kusaidiana na Waziri wetu Makamba kukifanya Kiswahili kitambulike huko twitter huu ndio ushirikiano sasa wa EAC
 
Lugha ya Taifa(National language) ni Kiswahili
Official language ni English na Swahili
sasa kama kiswahili ni lugha "yenyu" ya taifa, kwanini wengi "wenyu" huwa mnadhihaki kiswahili na kukitukuza kingereza?.

nimeshuhudua mara nyingi hapa jamiiforum mkijivunia kumudu kuzungumza kingereza na kujisikia fahari kana kwamba ni lugha yenu ya asili.

acha nikuchekeshe kidogo:
wakenya huwa "mnajitia" kumudu kingereza, halafu mkiwa kwenye matatizo mnazungumza kiswahili na kinawajia "automatically" bila kujua.

mfano ni pale mkenya anapopata ajari. akiwa katika harakati za kujiokoa katika ajari, huongea kiswahili.kingereza kinatoweka.

mkenya anapokabiliana na askari hasahasa askari wa barabarani. mkenya huongea kiswahili ili kutetea haki yake.kingereza kinatoweka.

mkenya anapokuwa na hasira. hapa ndio sisemi...kingereza kinasahaulika, "atabonga" kiswahili mpaka hasira zake zimuishe.kingereza kinatoweka.

mkenya anapodai haki yake pale anapohisi kadhurumiwa. hapa kingereza cha mkenya kinatoweka ghafla. atadai haki yake kwa kiswahili.

msicheze na kiswahili... hii lugha ina nguvu sana.
 
Waganda hawajui kiswahili hata kdg, are theyEast Africans?
 
Wazungu washafahm nyie ni mbwa koko kisw kinazungumzwa kwa ufasaha Tz...viazi vinalimwa kwa wingi Mbeya ila chips zinalika zaidi Dar, if you kno what I mean
I know what you mean. Wanaume wa dar wanapenda chips sana. 😀 Duh!
 
Mkenya wa kawaida anajua kuzungumza kiswahili zaidi ya kingereza.
 
Kiswahili kinachofunzwa shuleni kenya ni kiswahili fasaha.....ila Sheng ni Lugha ya mtaa, nikama pidgin ya Nigeria but bado wanajua English
 
Serikali yetu inapaswa kuchukua msimamo mkali kukuza kiswahili. Safaricom na kampuni zingine zipigwe marufuku kuweka adverts za sheng kabisa. Kwa runinga pia wasoma habari wa kiswahili na vipindi vya kiswahili vinapaswa kupewa mda mwingi kuliko kiingereza. Kiingereza sasa ata mtu ambaye ajaenda shuleni anakielewa manake kimejaa kila pahali kwa media na social media. Kiswahili ni lugha yetu sisi wakenya na naskia vibaya hatuipi ile sifaa na nafasi inayo faa.
 

Hatudhihaki Kiswahili, huwa tunachekelea wale Wabongo wanaojaribu kutype Kiingereza alafu wanabaki wamekiharibu ndio maana sisi huwaambia wabaki tu kwa Kiswahili sio kwamba tunakidhihaki bali tunawaeleza watumia lugha wanayoielewa ndio waeleweke. Hamna haja ya kung'ang'ana na lugha huelewi wakati unaweza eleweka kwa lugha nyengine.
 
hamna haja ya kung'ang'ana...

ilipaswa uandie "kung'ang'ania" na sio kung'ang'ana.

jifunze kwanza kuandika kiswahili fasaha na mujarabu halafu urudi kujadiliana na mimi. [emoji23] [emoji23]
 
So I marvel at the way KOT promote a cause...One hashtag can start a movement...Men I remember the CNN hotbed of terrorism hashtag...Literally got international recognition..

I think it was [HASHTAG]#Someonetellcnn[/HASHTAG]

Kiswahili kitukuzwe...bravo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…