:decision:Kwa mwanaume akimfumania mke wake akifanya uzinzi, anaweza kumshitaki huyo mwanamume mzinzi moja kwa moja mahakamani kudai fidia kwa tendo hilo. Upande mwingine mume au mke anaweza kwenda kulalamika dhidi ya mwanandoa mwenzake kwenye baraza la usuluishi la kata katika eneo analoishi lengo kubwa likiwa ni kutafuta usuluishi wa ndoa. Ikiwa mwanandoa huyo ataendeleza tabia hiyo na jitihada za usuluhishi zikashindikana, mume au mke huyo aliyefumania anaweza kwenda mahakamani kudai talaka.:decision: