Swali: baada ya kusafiri umbali mrefu, ni muda gani yapasa upite gari ndo izimwe.?

Mkuu upo sahihi kabisa hiyo ntaendelea kuamini hivyo maana ni dk kadhaa tuu na sipotezi kitu hapo...
 
Shkamoo Google translator...

Khaaaa!
 
Mkuu,niliwahi kusikia kua wakati wa Baridi fuel consumption ya Magari hua juu tofauti na siku za Joto!
Kuna ukweli wowote hapa?

Mimi kawaida uwa nawasha Beemer yangu sekunde 90 kabla sijaanza kutembea ili kuruhusu oil kuwa imefika kote inapopaswa kuwa
 
Mkuu unachoamini hata kama umeambiwa na mtaalamu wa Nit sio sahihi.
Under normal conditions hakuna part yoyote inayobadilika shape kutokana na joto la engine ., La sivyo tungepata blow by na extreme oil consumption when engine is hot ..engine parts zinatengenezwa na torelance kubwa sana ya joto .
 
Idea ya kuacha idle gari baada ya safari ni applicable kwa turbocharged engine tu. Japo kuna conditions zake
Turbo inapata lubrication kutoka engine oil, inapofanya kazi kubwa parts za turbo huwa zinapata joto Kali huku zikiwa katika mizunguzko mikali , unapozima gari katika hali hii ni kwamba. Unainyima turbo supply ya oil wakati ikiwa ya moto na mizunguzko mikali, kitakachotokea ni (Coking), kwamba oil chache iliyobakia kwenye turbo bearing itaunguzwa na turbo shaft ambayo inazunguka kuwa spidi huku ikiwa ya moto . , kiufupi huwa inaanza turbo kufa halafu inafata chain reaction flan amazing amabayo huja kuuwa engne pia.

Unaweza pia usiache idle gari hata kama umetoka kufanya kazi ngumu au safari ndefu,na usifanye uharibifu , Anticipation driving!! , Kama unaijua destination yako vizuri then km 5 kabla ya kumaliza safari endesha gentle Ili uruhusu turbo kupoa mizunguzko ,technically usiposikia muluzi wa turbo (turbo whistle ) basii jua turbo ipo katika mizunguzko michache .katika hali hii unaweza kufika na kuzima gari
 
Yes hata kuwe na baridi kiasi gani. Lakini kama thermostat imechomolewa gari haitakaa ifikie "engine operating temperature" kwa hiyo itabugia mafuta sana.
 
Iache gari silence kwa dakika 10-15. Hakuna unachopoteza isipokua muda na mafuta.
 
Salute mdau
 
Kwa engine natural aspirated Hakuna unacho gain pia
Unapoteza tu mafuta na pesa yako , in fact excessive idling pia ni hatari kwa afya ya engine.
Mkuu huwa nasikiliza sana ushauri wako ila kwenye hili wacha nipoteze tuu mafuta yaani nitoke umbali mrefu nifike nizime tuu gari labda hizi za kisasa sio zile zetu za new model ingawaje ni ya toleo la nyuma..bima, Hyundai, Audi ,Toyota hata Benz ya miaka ya karibuni ntazima tuu Ila sio zile za kitambo ukizima safari inaweza kuishia hapo hapo bora liwake tuu uendelee na saafari yako ndefu
 
Wengine wanasema ukiiacha gari idle kwa muda kidogo baada ya safari inasaidia oil kushuka...hili sijui limekaaje

Katika kuiwasha ndio logic ya oil inatumika maana ukiwasha gari unaiacha iungurume kwa dakika kadhaa ili oil iende sehemu zote lakini kwenye kuzima unazima tu maana itarudi katika sehemu yake yenyewe ukiiacha idle bado oil itakuwa kwenye system nyingine maana engine bado ipo ON.
 
huu uzi umenipa elimu sana, inanipasa kuamini kua kuna vitu vingi sana kuhusu magari mtaani tunaamini tunavijua kumbe tunachemka, thank to JF
 
Umeongea kitaalamu kabisa.

Hasa hiyo km 5 kabla ya destination.
 
Umeongea kitaalamu kabisa.

Hasa hiyo km 5 kabla ya destination.
Anticipation driving , kwenye gari za kisasa unapata hata scores the way you drive .
Mtu unaona kabisa taa au round about ipo mbele yake lakini bado anakomaa na acc Ili afinge breki akiwa pale ,
Dereva mzuri anaachia kukanyaga moto na gari linaserereka hadi linafika kwenye taa au round about na kusimamia au atatumia breki kidogo sana .
 
Mara nyingi kama destination ni kwenye mji lazima utapokelewa na vifoleni vya hapa na pale au mataa kabisa.

Mpaka unafika nyumbani kwako gari inakuwa imeshapoa vya kutosha.
 
Bodaboda je? Tuzime baada ya muda gani?
**kichwani Helmet, pua+mdomoni barakoa.
****Reflector jacket yaan tumeshakua father krismasi bila kupenda
Hahahaaa.. ahsante mkuu umenichekesha mpaka nimekunywa maji...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…