Swali fikirishi: Arsene Wenger ana tatizo gani, Hofu aliyonayo inatokana na nini?

Mtini

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
1,492
Reaction score
2,361
Kitu kitu sijakielewa vizuri kuhusu huyu Kocha wa timu yetu ya Arsenal, huyu mtu wa kwetu Aserne Wenger. Tangu nimemjua huyu Kocha nimeshuhudia akifanya mambo mengi makubwa kuhusu hii timu yetu. Baadhi ni kama haya
1. Amefukuza wachezaji wazembe na wavivu
2. Amepunguza gharama za uendeshaji wa timu kwa kutosajiri wachezaji wapya na wa gharama
3. Amepunguza sana faulo ndani ya uwanja
4. Amejenga miundo mbinu ya uwanja wetu wa nyumbani
5. Bila kusahau kahamisha makao makuu ya club
6. Na wewe unayesoma ongezea ya kwako

Kwa ufupi Arsene Wenger kufanya mambo mengi ya kishujaa ambayo watangulizi wake walishindwa. Ila ana tatizo moja, sijui linatokana na nini "ANAOGOPA SANA KELELE ZA MASHABIKI"
Tumeshamshauri Kocha wetu acha kuogopa mashabiki tumekupa mkataba wa miaka 5 Unaogopa nini, mashabiki hawa ni kelele tu hawana uwezo wa kuuvunja huu mkataba, tumeshamuhakikishia kuwa tunaweza muongeza tena miaka 2 kwenye mkataba wake ila bado kelele za mashabiki zinamtesa.

Labda mashabiki wa timu na benchi la ufundi mnisaidie "HOFU YA KOCHA WETU INATOKANA NA NINI? "
 
7. Karudisha nidhamu kazini. Woga wake hajiamini. Mimi siwezi kumulaumu kocha wetu!!! Nakilaum chama chake na bao la mkono.
 
7. Karudisha nidhamu kazini. Woga wake hajiamini. Mimi siwezi kumulaumu kocha wetu!!! Nakilaum chama chake na bao la mkono.
Na nidhamu ya wachezaji imerudi kabisa, hawapokei rushwa siku hizi
 
Wenger= magu. tatizo ni IQ na plagiarism
 
Hakutakiwa kuwepo kwenye hiyo nafasi, wakati wake wa mambo ya kiruga ruga ulishapita!

Na iwe fundisho kwa wanachama na wenye klabu kuwa makini wanapotafuta makocha
 
Katika wazee wenye jeuri hapa duniani basi mzee Venger yumo.. mie simwelewi huyu babu kuachia mikoba sijui anaona nini yani kila siku utaskia ahaadi zake, we gonna win the league,, we gonna win the league.. Sasa we goona win mpaka lin babuu #WENGEROUT
 
Anajua kuwa kuna kanuni za mchezo na yeye hazifuati.........
 
Hapo miundombinu ya uwanja wa nyumbani, ndiyo ile kitu ya kuitwa tocha internet nal.
 
Anaogopa kivuli cha maovu au uhalifu aliyofanya. Hakuna mwanadamu mkamilifu, yeye anataka kulazimisha kuwa yu kamili.
 
Wenger anaogopa kuachia ngazi Arsenal japokuwa anajua fika muda umefika, hana tena jipya amabalo atalileta ndani ya Arsenal, sasa woga wake mkubwa ni kwamba kwa miaka mingi aliyokaa na mafanikio aliyoipa Arsenal haviendani

So woga mkubwa ni kwamba atakuja kocha mwingine ndani ya muda mchache na anaweza kufanya mambo makubwa kuliko au kumkaribia yeye aliekaa miaka nenda rudi, kivuli cha alex ndio kinampa ugumu wa kuachia ngazi, mwenzie kwa muda aliokaa man u kaleta mataji mengi sana, kwa maoni yangu

Kwa maoni yangu wenger anahofu ya kuonekana hajafanya lolote japokuwa sio kweli, yeye kama kocha amefanya mengi ya kupewa sifa ila tatizo hajiamini, mchawi wa wenger ni wenger mwenyewe na hakuna kingine, muda wa kuiacha club umefika ye analazimisha tu
 
Tumpe muda huyu coach labda atatufikisha ktk matamanio na matatajio yetu shida kama unavyosema ni hofu tu japokuwa huyu pia muda aliokaa sio wa kutosha kama pacha wake wa Emirates
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…