Swali fikirishi: Inasemekana kipindi isaka anatolewa sadaka na baba yake ibrahimu Isaka alikuwa na umri wa miaka 34 je Isaka alikubali vipi?

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Wakuu unaposoma tu weweunadhani lilikuwa jambo rahisi sana .........soma kwanza

Mwanzo 22:1Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa.
2 Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.
3 Ibrahimu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu.
4 Siku ya tatu Ibrahimu akainua macho yake, akapaona mahali pakali mbali.
5 Ibrahimu akawaambia vijana wake, Kaeni ninyi hapa pamoja na punda, na mimi na kijana tutakwenda kule, tukaabudu, na kuwarudia tena.
6 Basi Ibrahimu akazitwaa kuni za hiyo sadaka, akamtwika Isaka mwanawe; akatwaa moto na kisu mkononi mwake, wakaenda wote wawili pamoja.
7 Isaka akasema na Ibrahimu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa?
8 Ibrahimu akasema, Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka, mwanangu. Basi wakaendelea wote wawili pamoja.
9 Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu, Ibrahimu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni.
10 Ibrahimu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe.


Ebu wewe kijana wa miaka kuanzia 15-30 uvae uhalisia wa isaka halafu mzee wako haijarishi ni mlokole kupindukia au uwe mtoto wa nabii wa sasa hivi hawa.Baba yako akumbie maneno yale mnafika eneo la tukio ghafla mzee wako anakukaba na kukufunga then anakulaza.

Je isaka alikubali vipi ili hali alimuuliza swali nyeti kabisa mzee wake kuwa "
Isaka akasema na Ibrahimu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa?
8 Ibrahimu akasema, Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka, mwanangu."


Kwanza tukubali ibrahimu alimwambia uongo mtoto kuwa Mungu atajipatia sadaka ili hali akijua vyema kabisa anaenda kumtoa sadaka mwanae.

Wakuu hii iliwezekana vipi maana kwa sasa hivi mzee hata eleweka kabisa na kipigo kitamuhusu hukohuko kwenye eneo la tukio.
 
Hivi hizi stories unahakikishaje zilitokea kweli na si hadithi za kuungaunga tu?
 
Sasa unafananisha kwamba vijana wa sasa hawakubali au wazamani wanakubali au nini unachotafuta wewe?
Katika Uyahudi – Baadhi ya wanazuoni wa Kiyahudi wanadai kuwa Isaka alikuwa na umri wa miaka 37 wakati wa tukio hilo, wakirejelea mafundisho ya Midrash na Talmud.

Wakristo wengi huamini kuwa Isaka alikuwa kijana mdogo, labda kati ya miaka 12 hadi 20, kwa sababu alionekana kuwa na uwezo wa kubeba kuni kwa ajili ya sadaka (Mwanzo 22:6).

Katika Uislamu, Ingawa Qur'an haimtaji moja kwa moja Isaka kama mwana aliyetolewa sadaka (wapo wanaoamini huenda lilikuwa ni tukio la Ismail), tafsiri nyingi za Kiislamu zinaeleza kuwa alikuwa kijana wa umri wa kubalehe au zaidi.

Isaka alikubali kutolewa sadaka kwa sababu ya utii wake kwa baba yake, Ibrahimu, na imani yake kwa Mungu. Ingawa maandiko hayatoi maelezo ya moja kwa moja kuhusu hisia zake, tunaweza kuelewa utii wake ukisoma mwanzo 22:1-14 na simulizi za Kiislamu.
So utii, imani yake kwa Mungu, na moyo wa kujitoa kwa ajli ya mapenzi ya Mungu na baba yake alivyofanya.

Na mwisho ambao wewe hujaandika ila ndio story nzima, Mungu alimzuia Ibrahimu na badala yake akatoa kondoo wa sadaka, akionyesha kuwa jaribio hilo lilikuwa la kuonyesha utii na imani, si lengo halisi la kumtoa Isaka dhabihu.
 
Narudi mkuu nilale kwanza
 
Hii habari inachanganya
Waislam wanasema hakuwa Isaka alikuwa Ismail na wakristo wanasema hakuwa Ismail alikuwa Isaka
 
No alikua yanki sana. Maybe miezi 34 sio miaka.
 
Kuhusu umri wa isaka sijui ila swali ni la kitoto ....maana kama ni mungu basi mungu ndiye anaye control nafsi za viumbe wote...kama mchawi tu anaweza kuchukua mtu mzima kabisa wa umri kuwa msukule akamfanyisha atakavyo sembuse Mungu kwa mwanadamu ....isaka itakuwa alikuwa ana kontrolewa na mungu ili Ibrahim ajaribiwe uaminifu wake.
 
...Jaribu Kutafakari TU....Kama Watu wa Agano la Kale waliweza kuishii Hadi Kufikis Miaka 700, yaani Mtu kuwa na Umri wa Miaka 700, Mtoto au Kijana alikuwa na Mika mingapi ? SI Inawezekana kabisa Mtoto Hadi Kijana alikuwa Mwaka 1 Hadi 75 ikiwa na maana ya Miaka 10 Hadi 15 Sasa hivi ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…