Huo ndio UKWELI wenyewe, kwa wanayotutendea hawa KENGE ilipaswa tukinukishe long time kitambo.
Ripoti za CAG ni madudu yasiyoelezeka, lakini tupo kimya, wachache tumeamua kuwa keyboard warriors, na walivyotuzoea sasa, likitokea la kutokea wanaleta habari MSANII DIAMOND ANA MIMBA😂🤣 tunasahau yote, sisi ni zaidi ya kuku ujue, wepesi kusahau, siku uwoga utakapoisha basi litatokea jambo, paka mgonge gonge lakini usimuweke katika hali ya HAKUNA NAMNA lazima ajitetee kwa mpambano ili aishi. Huu unafiki wa amani yetu sijui kimeenda kimerudi ni moja kati ya adui zetu wakuu, hakuna amani nzuri ya namna hii.
Level ya elimu ikiongezeka nadhani watu wengi watashtuka.
Mtaji mkubwa wa wanasiasa nchi ni UJINGA WETU SISI WADANGANYIKA.
Wanasiasa nchi hii ni kama miungu watu, wanafanya ya hovyo mengi mnoo