Nawasilimu wote [emoji120]
Kuna jambo nimekuwa nikitafakari kichwani muda mrefu sasa,ipo hivi kama ilivyo kawaida kila mtu ana njia yake ya kusaka riziki mfano wengine ni waajiriwa wa serekali na sekta binafsi wengine wamejiajiri.
Jambo ninalotafakar mimi kwa sisi waajiriwa ikitokea siku huna kibarua je utafanya nini unachomudu maishani mwako nachojiuliza mimi ni "what am l good at" kama wewe ni mwajiriwa au upo tu huna fani inayokuingizia shilingi mbili tatu ni vzr na wewe ukatafakar hilo jambo napenda kuwasilisha hoja asanteni kwa muda wenu .
majibu ya hilo swali hayawezi kulingana. Jibu sahihi zaidi utalipata wewe mwenyewe muhusika uliyejiuliza.
Mimi au mtu mwengine yoyote ni ngumu kujua wewe ni mzuri kwenye jambo gani au sekta gani. Ila kuna njia unaweza kuzitumia za kujua upo good kwenye kitu gani:- njia zipo nyingi hizi ni baadhi tu
1. Angalia jambo ambalo unapenda kulifanya mara kwa mara
2. Jambo ambalo ukilifanya huchoki kama ukifanya mambo mengine.
3. Jambo ambalo unafurahia kulifanya
Ukishapata hilo jambo jiulize je unaweza kupata kipato kupitia hilo jambo? Kama jibu ni ndio, je ni kwa namna gani?
Nadhani hapo unaweza kupata mwanga ni wapi pa kuanzia.
Mara nyingi pesa hupatikana kwenye changamoto, ukiweza kutatua changamoto kwenye jamii inayokuzunguka basi pesa itakufata tu.
Unaweza kuanzia hapo pia, angalia changamoto gani zipo mtaani kwako, ofisini, kijiweni au wilayani, au hata kwa mkoa. Sikiliza watu wanalalamika sana kuhusu nini? Igeuze hiyo inayoonekana changamoto kwa wengine iwe fursa kwako.
Jifunze namna ya kuitatua hiyo changamoto, namna inavyoweza kukupatia kipato. Jifunze kupitia watu
Pesa zipo, zipo mikononi mwa watu, zipo serikalini. Ili kuzipata lazima uwe na wazo sahihi. Na hilo wazo ulifanyie kazi kwa usahihi. Usichoke kujifunza vitu mbalimbali. Pengine jambo unalopenda kufanya ni ngumu kukuingizia kipato. Basi jifunze jambo jipya.
Hilo swali usichoke kujiuliza, jiulize hata mara elfu. Majibu utakayoyapata yafanyie kazi. Usipuuze hata wazo dogo kiasi gani, pengine wazo/jambo utakaloona la kipumbavu likawa na tija kubwa sana
Aaaah nimeandika sana, nahisi inatosha kwa leo. KARIBU SANA