Pre GE2025 SWALI: Ikiwa ndani ya CHADEMA pia kuna harufu ya rushwa, ipo haja ya kupata chama kingine cha upinzani wa Kweli?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!!

Haya pia ni madhara ya kubaki na chama kimoja kikuu cha upinzani.

Tukijiuliza jwa sasa, CHADEMA bado kina sifa ya kuitwa chama kikuu cha upinzani, wangapi watakubaliana na HOJA hii ikiwa RUSHWA inayotajwa na viongozi ndani ya chama?

Ok, Chadema wanashawishiwa kuhongwa, huyu mtu au kikundi cha watu toka chama tawala kinachojiamini kuhonga wanasiasa ni akina nani?

Ikiwa CHADEMA na CCM ndio vyama vikubwa kwa sasa na vinatoa harufu ya RUSHWA, je Kuna haja ya Kupata chama kingine cha tatu tukifanye kuwa chama kikuu cha upinzani?

Na chama hicho cha tatu ni kipi na nani wa kukisajili na kukijenga hadi kufikia hatua iliyofikiwa na CHADEMA?

Ama kweli, mbobezi wa kupiga mbizi, hufia pwani!!

Mungu ibariki CHADEMA iweze kuondoa harufu ya RUSHWA.

MUNGU ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Tundu Lissu: Kuna Rushwa inatuvuruga ndani ya CHADEMA
 
Yani kiongezeke chama kingine tena?🤣🤣
Sasa ikiwa matumaini yamekosekana CCM na CDM Si nikuondoka na kuanza UPYA?

Sasa mwenye HAKI atashirikiana vipi na mla RUSHWA.
 
Chama chotara kinatakiwa Kuzaliwa haraka.
 
Rushwa haikimbiwi bali huwa tunapambana nayo hapo ulipo sababu hakuna chama utahamia ambacho hakina.rushwa. we are all sinners the only problem is that we sin differently. Sasa the choice is yours however myself id rather choose the devil i know than an angel i dont know.
 
Ni kweli Chadema kuna rushwa inapenyezwa huwaoni akina Msigwa? Baada tu ya Lisu kusema ukweli huo Yuda Iskariote akaonekana. Kwahiyo ni kweli ipo. Na inatoka Kwa wataalamu wa rushwa. Kula Kwa urefu wa kamba ya kila mtu.

Ili kuisamaratisha Chadema Kwa akili ya kawaida kama unaweza kugawa Pikipiki 700 kila mkoa unashindwaje kuwanunua watu 10 mhimu Kwa milioni 500 kila mmoja? Halafu wapiga kelele wa CCM wa siku zote unawapa t-shirt na khanga wanaendelea kupiga makofi na kubebwa na Fuso kwenda mikutanoni?
 
Sasa ikiwa matumaini yamekosekana CCM na CDM Si nikuondoka na kuanza UPYA?

Sasa mwenye HAKI atashirikiana vipi na mla RUSHWA.

..vyama vikuu vya siasa vinatakiwa vilingane-lingane kiuwezo, kifedha, na kirasilimali.

..Wakati wowote ule uchaguzi unapoitishwa, tunatakiwa tusiwe na uhakika chama gani kati ya vyama vikubwa kitashinda.

..Kuanzisha chama kipya cha upinzani, ktk mazingira yetu ya kisiasa, na kidemokrasia, sidhani kama kutakuwa na matokeo mazuri.

..Kama Watanzania tumeshindwa kuviunga mkono vyama 22 vya upinzani vilivyosajiliwa sasa hivi, tuna uhakika gani tutaweza kukiunga mkono chama kipya cha upinzani cha 23?
 
Salaam, Shalom!!

Haya pia ni madhara ya kubaki na chama kimoja kikuu cha upinzani.

Tukijiuliza jwa sasa, CHADEMA bado kina sifa ya kuitwa chama kikuu cha upinzani, wangapi watakubaliana na HOJA hii ikiwa RUSHWA inayotajwa na viongozi ndani ya chama?

Ok, Chadema wanashawishiwa kuhongwa, huyu mtu au kikundi cha watu toka chama tawala kinachojiamini kuhonga wanasiasa ni akina nani?

Ikiwa CHADEMA na CCM ndio vyama vikubwa kwa sasa na vinatoa harufu ya RUSHWA, je Kuna haja ya Kupata chama kingine cha tatu tukifanye kuwa chama kikuu cha upinzani?

Na chama hicho cha tatu ni kipi na nani wa kukisajili na kukijenga hadi kufikia hatua iliyofikiwa na CHADEMA?

Ama kweli, mbobezi wa kupiga mbizi, hufia pwani!!

Mungu ibariki CHADEMA iweze kuondoa harufu ya RUSHWA.

MUNGU ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Karibuni.

PIA SOMA
- Kuelekea 2025 - Tundu Lissu: Kuna Rushwa inatuvuruga ndani ya CHADEMA

Two wrongs don't make a right.
Shutuma za uchukuaji wa hela chafu zinazowahusu viongozi watuhumiwa hazihusiani kabisa na CDM kama taasisi imara, makini na inayojotegemea. Bali zinawahusu viongozi hao kipekee.

Ujio wa chama kipya utakuwa na tuhuma hizi hizi zinazoendelea ndani ya vyama vya kisiasa. Viongozi wengi siyo watu safi na wenye hofu ya Mungu. Wengi wao wapo ndani ya vyama kutokana na maslahi binafsi, na wala siyo maslahi mapana ya taifa.

Kwa hiyo basi ujio wa chama kipya na kikuu cha upinzani hakiwezi kuwa suluhu ya changamoto za sasa zitokanazo na tuhuma mbalimbali zinazowakabili viongozi wapendwa rushwa.
 
Sasa kama viongozi wa juu wanatuhumiwa RUSHWA,watawezaje kukemea kwenye chaguzi na mifumo Yao?
 
..vyama vikuu vya siasa vinatakiwa vilingane-lingane kiuwezo, kifedha, na kirasilimali.

..Wakati wowote ule uchaguzi unapoitishwa, tunatakiwa tusiwe na uhakika chama gani kati ya vyama vikubwa kitashinda.

..Kuanzisha chama kipya cha upinzani, ktk mazingira yetu ya kisiasa, na kidemokrasia, sidhani kama kutakuwa na matokeo mazuri.

..Kama Watanzania tumeshindwa kuviunga mkono vyama 22 vya upinzani vilivyosajiliwa sasa hivi, tuna uhakika gani tutaweza kukiunga mkono chama kipya cha upinzani cha 23?
Katiba ingetamka viwepo vyama VITATU pekee nchini,

Vipewe ruzuku, view sawa, visaidiwe kufika Nchi nzima, kuwepo na Utaratibu wa kupokezana madaraka kama US na UK.
 
Kwamba hicho kipya ndo kutakua hakuna fukuto la rushwa. Sahauni hilo.

Tubaki hapa hapa. Kazi kidogo, rushwa kidogo, Uzalendo kidogo, Unafki kwa sana
 
Katiba ingetamka viwepo vyama VITATU pekee nchini,

Vipewe ruzuku, view sawa, visaidiwe kufika Nchi nzima, kuwepo na Utaratibu wa kupokezana madaraka kama US na UK.
Uko sahihi mkuu. Utitiri wa vyama vya siasa, sio uti wa maendeleo kwa nchi maskini.

Kwanza mostly vyama vingi havina hata sera za kuelezeka
 
Sasa kama viongozi wa juu wanatuhumiwa RUSHWA,watawezaje kukemea kwenye chaguzi na mifumo Yao?
Wanaweza tu.

Magu mwenyewe alikua ananunua wapinzani, uchaguzi ukiisha anaaanza kupiga spana wala rushwa 😄

Kila kitu na wakati wake
 
RUSHWA ndiyo chanzo Cha Umaskini wa Watanzania,

Tusiichekee Wala kuizoea, itatunaliza.
 
Ishu iko hivi:

Jamii yetu yote imeoza. Inatukuza mafisadi. Yanaitwa majanja matoto ya mjini. Ukiwa mwadilifu utaitwa mshamba. Na ukiingilia ulaji wa watu utakolimbwa.

Hata hao viongozi wa vyama vya upinzani nao ni za la jamii hii hii mbovu. Siyo malaika. Hao waadilifu kabisa kabisa kama Nyerere utawatoa wapi katika jamii ya namna hii?

Kwa hivyo kutegemea chama kingine cha upinzani ni kupoteza muda tu. Cha kufanya pengine ni kuangalia yupi ni mwenye angalau unafuu kidogo. Ambaye atakula huku anasukuma maendeleo japo kidogo.

Kwa maoni yangu ningependa kumjaribu Lissu. Tuone kama atatuletea katiba mpya ambayo ndiyo hatua ya kwanza katika kujaribu kurekebisha mifumo yetu. Katiba impunguzie rais madaraka na imwondolee kinga. Tena itaje adhabu ya mafisadi kuwa ni kufungwa maisha bila parole na kisha kutaifishwa mali zote walizoiba hata wawe wamezificha wapi. Ndicho walichofanya ANGOLA na wameanza kupiga hatua.

Hatuhitaji chama kingine cha upinzani. Tunahitaji mtu mwingine mwenye uthuhutu atakayejitoa mhanga maisha yake. Angalau tu ajitahidi safari hii atuletee katiba mpya ya wananchi kabla hawajamkolimba!
 
Back
Top Bottom