Swali Je, Benki Kuu na Wizara ya Fedha zinachukua hatua gani kukuza ufahamu wa Fedha kuongeza Financial Inclusion?

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Moja kati ya kazi kuu ya Benki Kuu ni kudhibiti uchumi kazi ambayo inataka uwepo wa washiriki kwa ngazi zote ili maamuzi ya Benki Kuu yaweze kuwafikia wananchi wa kawaida amba wanaaswa kuwa washiriki

Soko la Fedha ndio tegemezi kubwa la Sera ya Fedha, ni wazi kuwa wananchi wakiwa wengi katika ushiriki wa soko la fedha ndivyo Sera ya fedha inavykuwa na ufanisi mkubwa. Maendeleo ya masoko ya fedha yamekuwa makubwa(Relatively) na kuleta ushiriki mkubwa wa wananchi lakini bado kuna shida ya ushiriki kama CMSA walivyokiri kwenye ripoti yao (Capital Markets and Securities Authority (CMSA), 2017-2018)

Changamoto zinazoonekana ni pamoja na Watu kutokuwa na ufahamu wa masuala ya fedha kiasi cha wengi wa kutaeliwa na mikopo umiza kama inavyothibitika hivi sasa

Aidha taasisi za kifedha zimejikuta zikijipa majukumu ya kuelimisha raia kuhusu masuala ya fedha, ikiwemo uhitaji na matumizi ya mikopo kabla ya kutoa, suala hili sio tu linaongeza gharama kwa benki au microfinance Institutions bali pia linakuwa la kukera kwa kuwa muda wa kupata mkopo unaongezeka na hivyo inakuwa ni inconvinient kwa wahitaji

Uwepo wa nyumba nyingi zisizoisha au miji isiyopangika ni suala la wazi kuwa mortagage bado haifanyi vizuri. Taasisi na watu binafsi kukopa nje, ni suala ambalo linaweza kuashiria vitu kadhaa, eidha hakuna ukwasi kwa benki, Masharti na gharama zilizopo ni kubwa relative na cross crediting, au dhamana za serikali hazifanyi vizuri kwenye soko la upili au yote

Uwepo wa watu wanaoikubali mikopo umiza ni ushahidi tosha kuwa watu wanapenda kuwa washiriki wa soko la fedha, lakini hawana ufahamu nalo. Wizara ya fedha, Benki Kuu, CMSA na DSE wanaathirika kwa namna moja au nyingine kwa wananchi kukosa ufahamu wa masuala ya fedha

Lakini imedhihirika idadi ya vijana wanaojaribu kuwa Arbitrageurs kwa kucheza FOREX hii yote ni uthibitisho kuwa washiriki wapo lakini hawashiriki kwenye soko sahihi, aidha kwa kutohesabu vizuri kiwango cha risks kwenye kila soko wanaloshiriki

Ni vyema serikali ikawa na mkakati wa wazi wa kufanya tafiti wa kuona kwa nini soko la fedha halifanyi vizuri na kuja na mkakati wa kulifanya lifanye vizuri.

Muandishi wa makala haya anasema, mashindano ya CMSA na DSE yanatoa ufahamu kwa vijana wa chuo ambao kwa Tanzania wengi wako na dissaving kama tukitumia nadharia ya Life Cycle (LCH)

Kwa sababu hiyo tunapaswa kujua muelekeo wa serikali kwenye kuongeza ushiriki (Financial Inclusion)

Signed

OEDIPUS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…