Swali: Je Chadema wanaweza kufungulia jeshi la polisi mashtaka mahakamani?

Jumanne Mkota

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Posts
2,987
Reaction score
1,757
Salaam wadau Nauliza kwa nia njema kabisa. Haya mambo ya polisi kukamata kamata viongozi wa chedema tena kwa njia dhalili hayawezi kukomeshwa? Na kama inawezekana ni vipi viongozi wangu wa Chadema wasikomeshe udhalimu huu? Nawasilisha kwa michango chanya cc. wanasheria wote members humu
 
Hawawezi.

Wamevunja sheria makusudi ili wapate umaarufu wa kisiasa...
 
Wanaweza kabisa kuwashitaki ndio maana polisi kwa kesi ya Iringa eti wakitafutwa wataitwa wanashindwa kusema tumewasumbua kwa sababu hawakuwa na hoja
 
Hivi mmeshawahi kusikia hata moja Zitto kakamatwa na polisi?
Siasa za kistaarabu ni kipaji, sio kila mtu anaziweza.
 
Hawawezi. Wamevunja sheria makusudi ili wapate umaarufu wa kisiasa...
Ndio maana na viongozi wa CCM huwa wanafanya makusudi ili wapate umaarufu wa Kisiasa kama vile 1. CCM kuzidisha muda katika mkutano wao pale Jangwani hadi saa 12.20 lakini kwao ilikuwa halali. 2. Aden Rage kuonyesha Bastora Hadharani wakati wa kampeni harafu akahukumiwa kulipa faini pekee kinyume na sheria 3. Ukiwaona Ditopile Mzuzuri (R.I.P) kuuwa kwa makusudi kwa bastora na kuwa nje kwa dhamana na kutohukumiwa, lakini Mungua akaona dunia haikutenda haki yeye kwa mapenzi yake akamuua 4. Andrew Chenge kuwagonga kwa makusudi wale mabinti na kuwaua na mwisho wa siku akahukumiwa kulipa faini Nayaandika haya kwa sababu akili yako inaonyesha wanaofanya makosa ni viongozi wa CHADEMA pekee huku wale waliopo CCM wao sheria wanzivunja na kuhukumiwa kinyume na haki ya sheria inavyotakiwa kuhukumu
 
Mkuu, kitendo cha viongozi wa chadema kwa siku za karibuni kukamatwa hovyo knatokana na viongozi wenyewe kuvunja sheria kwa makusudi ili waonekane mbele ya jamii kuwa wanaonewa
 
ZeMarcopolo;
Hivi mmeshawahi kusikia hata moja Zitto kakamatwa na polisi?
Siasa za kistaarabu ni kipaji, sio kila mtu anaziweza.

Acha Uzuzu Ww ZITTO alikamatwa Mwaka Jana SGD kwasababu Hizi hizi za kuzidisha muda kwenye mkutano uliofanyika STEND YA ZAMANI..
 
Wafungwa watarajiwa wanashtaki Mfungaji?
Hao wamekalia kuti kavu, wapigwe miaka 20 jela watajifunza.
 
Hawawezi.

Wamevunja sheria makusudi ili wapate umaarufu wa kisiasa...

natamani wakamatwe kila mara ili wazoee kwani mziki wa 2015 vikosi vyote ccm itaamuru idhibiti chadema.
kama si chadema tusingepata katiba mpya!
 

Sisi tunaoamini mabadiliko tunaona hizi ni opportunities.....ref Karl Marx, let nature take place, we do to fit in it, then we conquer it easily, dont fight it..fit in it...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…