Swali:Je walimu waligoma kuonyesha kuwa wanaweza kufanya hivyo au ?

Swali:Je walimu waligoma kuonyesha kuwa wanaweza kufanya hivyo au ?

Boligado

Member
Joined
Jan 10, 2012
Posts
44
Reaction score
49
Nimesikia katika taarifa kwenye radio kiongozi wa CWT anazungumza kuwa'tulipenda pia kuonyesha serikali na sisi(CWT) tunaweza kudai maslahi yetu kwa njia ya mgomo.' Mi sijaona tija yoyote kwa huu mgomo labda ilikuwa janja ya viongozi wa CWT kuendelea kujijenga kwenye chama na kuandaa mazingira ya kuchaguliwa tena. Maoni yenu katika hili.
 
baada ya mahakama kutoa hukumu na CWT kutoa tamko kukubaliana na kila kitu including kulipa fidia kwa wanafunzi (iwapo serikali itataja kiasi cha fidia hiyo), ni ngumu sana kujua kama CWT walikuwa wanajua wanachokifanya au waliamua kutangaza mgomo kichwa kichwa bila kwanza ku-establish uhalali wa mgomo huo kisheria na athari zake
 
Walimu mkuu hawawezi kuweka mgomo wa maana hadi kikaeleweka kwani wengi wao wameiona hiyo kazi ndiyo mwokozi wao hata kama hawalipwi vizuri kwani hii ndiyo kazi pekee unayoweza kuipata hapa TZ ukiwa umefaulu kwa division 4 point 28.Yaani hii kazi imezitangulia tu kazi za House maid na Bar maid.
 
baada ya mahakama kutoa hukumu na CWT kutoa tamko kukubaliana na kila kitu including kulipa fidia kwa wanafunzi (iwapo serikali itataja kiasi cha fidia hiyo), ni ngumu sana kujua kama CWT walikuwa wanajua wanachokifanya au waliamua kutangaza mgomo kichwa kichwa bila kwanza ku-establish uhalali wa mgomo huo kisheria na athari zake

Mkuu, wakati watu wametangaza huu mgomo mi nilisema humu jamvini kuwa "watu wanachezewa akili"
na dalili zote zinaonesha hivyo.
Humo ndani kuna watu walifanya hivyo kwa maslahi yao wanayo wajua wenyewe.
Tusubiri filamu nyingine.
 
Back
Top Bottom