GE2025 Swali Kabla ya Oct. 29: Waandamane au Wasusie Kura ya Urais?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kwani wizi wa kura CCM wameacha siku hizi?
Wataiba sema nina imani Watanzania wengi sana hawatopiga kura lwenye huu uchaguzi lakini pia Wabongo hawaaminiki unaweza kushangaa wakatoka kwa wingi.
Ogopa sana mtu anayeshabikia mpira 24/7 huku mlo wake ni wakubabisha.
 
Pata picha Samia anachaguliwa kwa kura milioni tatu tu katika nchi yenye watu zaidi ya milioni 60!
Ili achaguliwe kwa kura million 3 ni endpoint wote waliojiandikisha watajitokeza kupiga kura na kumpigia Mwajuma, wasipo jitokeza, kura zao zote zinapigwa na kupewa yeye, hivyo utashangaa ushindi wa kishindo atakachopata!.
P
 
Wataiba sema nina imani Watanzania wengi sana hawatopiga kura lwenye huu uchaguzi lakini pia Wabongo hawaaminiki unaweza kushangaa kwa wingi.
Ogopa sana mtu anayeshabikia mpira 24/7 huku mlo wake ni wakubabisha.
Adui wa CCM ni teknolojia najua siku hiyo watazima mitandao kama ilivyotokea 2020 kwa waishio Tanzania , hivyo watanzania wanatakiwa kuelekezwa njia nzuri ya kuchukua video na picha na kuzitunza vizuri.

Nina uhakika kama sio tarehe 28 jioni basi ni 29 mitandao itafungiwa tena halafu akina Pascal Mayalla watatumwa kusema watanzania wengi kwa sasa wana smartphone hivyo walikuwa wanafuatilia uchaguzi mitandao ikazidiwa.
 
Ili achaguliwe kwa kura million 3 ni endpoint wote waliojiandikisha watajitokeza kupiga kura na kumpigia Mwajuma, wasipo jitokeza, kura zao zote zinapigwa na kupewa yeye, hivyo utashangaa ushindi wa kishindo atakachopata!.
P
Ushindi feki wa kishindo wala haunikoseshi usingizi.

Kitakachonikosesha amani ni watu kujitokeza kwa wingi kuhalalisha upumbavu.
 
Pata picha Samia anachaguliwa kwa kura milioni tatu tu katika nchi yenye watu zaidi ya milioni 60!
That's exactly my point.. bora kampeni ingekuwa yabkususia uchaguzi wa Rais kuliko maandamano...ila labda hawa Gen Z watatushangaza
 
Mtu anapotoa maelekezo kama haya wewe utakuwa wa kwanza kuwasha kiberiti?
 
Ili achaguliwe kwa kura million 3 ni endpoint wote waliojiandikisha watajitokeza kupiga kura na kumpigia Mwajuma, wasipo jitokeza, kura zao zote zinapigwa na kupewa yeye, hivyo utashangaa ushindi wa kishindo atakachopata!.
P
Wangapi wamejiandikisha kupiga kura??
 
Ushindi wa Rais na wabunge wa CCM hautegemei kura. Hiyo ni geresha tu. Hata wakipiga kura watu wa tano bado rais na wabunge wata tangazwa kwa kura nyingi. Idadi ya kura tayari imesha andaliwa kwa kila kituo.

Kwa hiyo hilo la kususia kupiga kura haliwezi kuwa tatizo kwa CCM.
 
Wangapi wamejiandikisha kupiga kura??
Watu milioni 37.
The game ya riging inaweza kufanyika only waliojiandikisha, wasipo jitokeza
Zile ballot voting papers zote ambazo hsazikutumika, yaani wenyewe hawakujitokeza, watu wajifungia mahali salama, wanazitiki zote na kudumbukiza ndani ya masanduku ya kura as if zimepigwa.
P
 
bandiko zuri sana nafikiri wakiamua Kususia itakua bora zaidi kuliko kuandamana Rasi hata akiwa madarakani atajua ukweli
Kwa hawa wahuni walipofikia, hawa heshimu katiba wala sheria, hata hasipotekea mtu mmoja kupiga kura, wata mtangaza ameshinda tena kwa kishindo…hii ndo Tanzania ilipofikia…kama mtu anatekwa mahakamani unategemea nn.
 
Kulithibitisha hilo la kura nyingi hata kama watakaojitokeza kupiga kura ni wachache, nimekubaliana na rafiki yangu mmoja ambaye yupo team moja ya waangalizi wa kutoka nnje, kutumia CCTV camera (kwenye majengo matatu ambayo camera zimeelekea kwenye vituo vya kupigia kura)kurekodi uingiaji na utokaji wa wapiga kura na kuambatanisha rekodi hizo tatu kwenye ripoti yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…