Swali Kuhusu Import Clearing and TRA Taxation

PlanckScale

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2008
Posts
550
Reaction score
169
Wandugu,

Nimekuwa nikikomboa mizigo toka nje kupitia kwa Clearing Agent wangu.
Jinsi ilivyo, agent anapewa jukumu kisheria kushughulikia hiyo process kwa niaba ya mteja.
Kwahiyo basi, TRA wana communicate makadirio ya kodi moja kwa moja kwa agent.

Sasa mimi kama mteja nitawezaje kujua hiyo kodi ni kiasi gani bila kumtegemea agent wangu. Maana kwa sasa agent ndie anaye niambia "lipa kiasi hiki". Iniwezekana ana nichomekezea 🙁.

I need away of knowing the estimated tax independent of the clearance agent.
Is there away to contact TRA directly using my TIN.


Nifunzeni nijilinde,


Thanks
 
hapo kama unamhofia agent wako basi ni bora kutafuta mwingine. Maagent wanasajiliwa na TRA na hata applications ya TIN namba zao zina features zaidi ya TIN ya kawaida au ya mteja kwenye mitandao ya kodi.
Hii ni kwa sababu maagent ndio wana access ya moja kwa moja kwenye mitandao kama Asycuda++, TRA-PAD, ASYSCAN na mingineyo na wamewekewa bond endapo mteja anayemhudumia mizigo yake italeta matatizo.
Kuna vitu ambavyo unaweza kujua ushuru wake kabla ya kulipia mfano kama magari lakini mizigo mingine hata maagents wenyewe wanategemea TRA ndio watoe bei halisi.
Kuhusu hili la kijua malipo, inawezekana maana kwa wale wanaolipa domestic revenue unaweza kusajili mawasiliano yako na pale TIN yako inapofanya malipo unataarifia kupitia mtandao automatically.
 

Kuhusu hili la kijua malipo, inawezekana maana kwa wale wanaolipa domestic revenue unaweza kusajili mawasiliano yako na pale TIN yako inapofanya malipo unataarifia kupitia mtandao automatically.

Naomba ufafanue zaidi una maanisha nini hasa...

Mimi nataka kujua kodi bila kupitia kwa Agent when TRA wakisha fanya makadirio yao...Sio tuu kuambiwa na agent.
Maana agent anaweza fanya dili na mpokea malipo ndani ya benki (nisha shuhudia hayo!)
 
Naomba ufafanue zaidi una maanisha nini hasa...

Mimi nataka kujua kodi bila kupitia kwa Agent when TRA wakisha fanya makadirio yao...Sio tuu kuambiwa na agent.
Maana agent anaweza fanya dili na mpokea malipo ndani ya benki (nisha shuhudia hayo!)


Mkuu inawezekana kujua kabisa. Ni hesabu ndogo tu inahitajika pale. Muhimu ni kujua item unayoagizia inaangukia kwenye kundi lipi la aina ya ushuru unaotakiwa kulipia. so ukifahamu value ya mwisho ya makadirio kutoka TRA then kujua kodi kiasi gani inatakiwa kulipiwa ni rahisi tu kiongozi.
 

Asante mkuu, lakini swali langu sio jinsi ya kupiga hesabu. Hiyo simple.
Swali langu ni kuhusu channel ya direct communication kati ya mlipa kodi wa import na TRA.
Nawezaje mimi kama importer kujua exaclty what TRA wanataka nilipe bila ya kuambiwa through agent wangu?
Jee kuna namba ya kupiga, au kuingia kwenye mtandao nika weka, for example TIN number yangu na reference ya mzigo, kisha nika pewa jibu (direct from TRA)?

Unajua ukimtumia agent basi yeye ana communicate direct na TRA alafu ana kwambia lipa kiasi kadhaa. Sasa mimi kabla sija lipa nataka nijue jinsi ya kuwa contact TRA na kudaouble check hilo kisio. Jee huo uwezekano upo?
 
Weka wazi unaagiza nini isije ikawa kama kagame kaagiza silaha yeye akasema ni ma foil watu wakapiga chenji kota au kujifanya muhando unaagiza box la misumari na kusema ni spare parts.
 
Inabidi uwe unam monitor agent wako through daily status reports.. Also kodi siku hizi inakuwa calculated direct from Asycuda system so agent anatakiwa akutumia Asycuda++ documents inayoonesha kodi iliyooneshwa na system.. Usiruhusu agent akupe maneno mengi..

Binafsi simshauri mtu yeyote kutumia agents wa mitaani wasiojua wanachofanya,, ni bora shipment zako uruhusu zifanyiwe clearance na agent wa uhakika kama DHL, Kuhne+Nagel au SDV/ bollore africa logistics hizi kampuni zipo dunia nzima zinalipa wafanyakazi wake vizuri na wanafanya kazi kwa target bila longo longo kama ma agent wa mitaani.. Wakichelewesha mzigo storage wanalipa wenyewe mteja hauiingii hasara.. Japokuwa charges zao ndefu
 

How do you access Asycuda system? Au inabidi nipate print out kutoka kwa agent?
Kummonita agent hiyo siyo ishu. Again, what is important is to have the ability to access TRA information independent of the agent so I can compare the notes, so to speak.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…