Swali kuhusu ma-fumanizi, na reaction za wafumaniaji!

Aaronium

Senior Member
Joined
Oct 31, 2011
Posts
129
Reaction score
9
Wajameni nifafanulieni kisheria, je, fumanizi ni kosa? na udhalilishaji unaofuatia matukio haya, mfano kuwatembeza wahusika wakiwa uchi, kuwalazimisha kuwapiga picha wakiwa uchi, pengine kuwapa adhabu hizo na zingine kama vipigo, ufafanuzi wake kisheria umekaa vipi hapo?!
 
Kufanya mapenzi nje ya ndoa sio kosa la jinai kisheria au kifanya mapenzi na mtu yoyote ambaye ni over 14 sio kosa kisheris hivyo fumanizi sio kosa.

Vitendo vyovyote atakavyofanyiwa aliyefumaniwa iwe ni vya udhalilishaji au shambulio la kudhuru mwili, mtu huyo anayo haki ya kufungua mashitaka ya jinai na pia kufungua kesi ya madai kudai fidia!.

Mwenye mali kama kamfumania mkewe, then ana haki ya kumfungulia kesi ya madai mgoni wake ili amfidie mali zake alizo mlia.

Ikitokea kukafanyika mauji kwa aliyefumania, then muuaji kama ndio mwenye mali na ndie aliyefanya mauaji kwa ama mgoni wake ama wote wawili, atashitakiwa kwa mauaji ila anaweza kushinda kesi kwa utetezi wa provocation kuwa wakati akifanya kitendo hicho, hasira zilimpanda sana mpaka akili zikamruka na kuua lakini baada ya mauaji akili zikamrudia na hivyo kujuta kwa kitendo hicho. Mtuhumiwa huyo ataachiwa huru kwa insanity kwamba wakati anaua hakuwa na akili timamu kufuatia provocation iliyosababisha pseudo insanity!.
 

Umeongea vema sana mkuu, ila tuwakumbushe wadau kuwa hakuna utetezi utakaokubalika kisheria kwa jinai haswa "Mauaji"
yaliyotokana na fumanizi endapo itabainika kuwa yalikuwepo maandalizi ya fumanizi husika. wale wanawapiga picha wenzi wao
mara nyingi huwa wamefanya maandalizi, hivyo hutenda makosa ya jinai kwa vitendo vyao vya kudhalilisha wagoni.
HATA HIVYO NAWASHAURI WATUNZI WA SHERIA WALETE SHERIA YA KUUFANYA UGONI KUWA KOSA LA JINAI, ITAPUNGUZA
IDADI YA MAUAJI. Endapo wanaofumania watapata fursa ya kuwapeleka Polisi Wagoni wao itasaidia, hivi sasa watu wengi huzikwepa taratibu ngumu za sheria ya madai hivyo hasira zao hupelekea mauaji.
WITO: hakuna haja ya kuuana kwani "ASALI HAINA MAKOMBO"
 
 
NAOMBA KUKUJIBU KISHERIA KAMA IFUATAVYO-
1. fumanizi ni HAKI YA MUME AU MKE KATIKA NDOA- nalo linaitwa ugoni, ukimkamata mwizi wako unawezz kumshitaki mhakamani na kulipwa fidia kwa tendo hilo

2.udhalilishaji ni kosa kisheria, kwani sheria inazuia mtu kutembea uchi au kutembezwa uchi au kuwapiga picha wakiwa uchi au kufanya matendo ya namna ya picha za ngono au vitendo vya ngono hadharani, ndio maana kila mtu anahesabika kuwa hana hatia hadi pale anapokuwa na hatia na mahakama

3. kumpiga mtu kisheria ni kosa na linaitwa 'assault, mtu akishitakiwa akatiwa hatiani atapigwa faini au kufungwa kifungo jela

hivyo, ni kweli inauma kuibiwa mke wako lakini si dhani kama ni busara kuwafanyia matendo hayo. kwa bahati mbaya wengine hata sio wake zao bali wazinzi wenzao au waasherati tu ambao ni kinyume na biblia
 
kuna jamaa amekamata msg za simu za kimapenzi kwa mke wake, je nao anaweza kuufanya amekamata ugoni?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…