Swali kuhusu masters degree

the-true-wash

Senior Member
Joined
Oct 14, 2012
Posts
142
Reaction score
109
Habari wadau.
Nina mpango wa kuanza kusoma MBA mt. Meru university lakini mbona watu wanaponda saana hicho chuo?
Kwani ukiwa na masters je inatofautishwa kwa chuo ulichosoma au??
Msaada jamani maana vyuo vingine ada ni juu sana.
 
Kwa uwezo wako naona hicho chuo kinakufaa. tusikulaZimishe kusoma vyuo vinavyokuzidi uwezo bure. Nenda kasome utamaliza bila supp si ndio unachotaka?
 
Siongelei supp wala uwezo.
Nataka kufahamu kama masters ya chuo flan ni zaidi ya masters ya chuo kingine kwa kozi moja.
 
Kama umeshindwa kujibu kaa kimya?
Badala ya kujibu swali unaleta upuuzi tu
 
Habari wadau.
Nina mpango wa kuanza kusoma MBA mt. Meru university lakini mbona watu wanaponda saana hicho chuo?
Kwani ukiwa na masters je inatofautishwa kwa chuo ulichosoma au??
Msaada jamani maana vyuo vingine ada ni juu sana.

Achana na wanayosema watu. Wewe unaetaka kusoma ndiye unayepaswa kuchagua chuo unachodhani utafanikiwa kusoma na kumaliza. Kwa maana hiyo ni juu yako kufanya utafiti kati ya vyuo mbali mbali na si kutegemea wanayosema watu kwakuwa wao sio wanaokwenda kusoma.
 
Siongelei supp wala uwezo.
Nataka kufahamu kama masters ya chuo flan ni zaidi ya masters ya chuo kingine kwa kozi moja.

The answer to your question is obvious!

Hapo wanagawa marks. Tena kama wewe ni Mbaptist, udini ni sehemu yake hapo.
 
Kasome bwana. Mbona zipo shule za kata watu wanasoma na wanafaulu vizuri?
First class inakusubiri hapo, kaichukue faste.
 
Siongelei supp wala uwezo.
Nataka kufahamu kama masters ya chuo flan ni zaidi ya masters ya chuo kingine kwa kozi moja.
Kama huu uchunguzi tu unakusumbua!!!!
Thesis utaandika???!!!!
Kwani masters ni nini haswa!!!
 
Huwa nashindwa kuwaelewa kabisa watanzania wenzangu!~ Jamani, sasa hivi tupo kwenye Globalisation world, then wewe unang'ang'ana na elimu ya 20th century, why?

We have moved from 20th century, 21st century, new millennium now Globalisation, lakini watu bado mnafikiri na kutenda ki-20th century.

Hivi yale makampuni ya Gas na Mafuta kule mtwara yakikunyima kazi na kumpa m-Kenya utayalaumu?
 
habari wadau.
Nina mpango wa kuanza kusoma mba mt. Meru university lakini mbona watu wanaponda saana hicho chuo?
Kwani ukiwa na masters je inatofautishwa kwa chuo ulichosoma au??
Msaada jamani maana vyuo vingine ada ni juu sana.
kama kuponda mbona kuna watu wanaponda hadi udsm mkuu?.kwenye ajira hakuna mambo hayo.kwenye ajira si kuna interview?na interview wanaita watu wote si wa kutoka vyuo fulani.
Ila kuna baadhi ya waajiri wanaangalia chuo pia ili kupunguza waombaji alafu mchujo unafuata maana wana assume chuo fulani ni macompetent.
Lakini kama unawasiwasi nenda kapige esami, udsm basi au mzumbe hao kwa mba wanatoa sana na watu wengi wanapendelea huko.ngoja na wengine watoe mawazo
 
Kwa uwezo wako naona hicho chuo kinakufaa. tusikulaZimishe kusoma vyuo vinavyokuzidi uwezo bure. Nenda kasome utamaliza bila supp si ndio unachotaka?

hivi ku-supp ni tatizo? unataka kuniambia mwanafunzi ambaye hajawahi ku-supp daima ni bora kuliko aliyewahi ku-supp?
 
We soma hapo hapo mt meru ndo level yako.
 
Kama huu uchunguzi tu unakusumbua!!!!
Thesis utaandika???!!!!
Kwani masters ni nini haswa!!!

nafikiri thesis ataandika tu sababu atafundishwa na walimu wa chuo atakakachojiunga. au kuna chuo kinacho-offer masters hapa tz ambacho siyo accredited?
 
hata kama chuo kimesajiliwa ni vyema kuwa makini kabla ya kujiunga na chuo husika. mfano kuna vyuo ambavyo kozi za masters zinafundishwa na wahadhiri wenye masters degree, hii nadhani sio sahihi kitaaluma.
 
Kwa uwezo wako naona hicho chuo kinakufaa. tusikulaZimishe kusoma vyuo vinavyokuzidi uwezo bure. Nenda kasome utamaliza bila supp si ndio unachotaka?

So ww utataka akamalize akiwa na sup. Yaan watanzania lini tutaacha ulimbukeni wa kudhani watu wakisup sana hapo ndio kuna shule ngumu? Mbona shule za sekondar watu wakiferi lawama huenda kwa walimu kuwa hawafundishi.sasa kwanin mtu akisup chuo ndio ionekane kuwa hicho chuo kiko vizuri?
Mm nadhan mshauri tu huyo jamaa kuwa chuo anachotaka kwenda kusoma masters yake bado ni kichanga hasa kwenye masters na hivyo ni vizuri angeenda kusoma kwenye vyuo vyenye uzoefu km mzumbe, udsm, saut, nk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…