Swali kuhusu mtoto

SHAROBALO

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2011
Posts
771
Reaction score
349
Habari

Naomba msaada juu ya HILI.

Eti mfano wewe umehangaika kupata mtoto muda mrefu sana na hatimaye.. mungu ameamua kukupa mtoto ila akakwambia uchague kati ya haya

1)Akupe mtoto mwema ambaye ni mchamungu na mtiifu ila ataishi kwa miaka ishirini tu atamchukua yaani atafariki.

2)Akupe mtoto mtukutu,asiyependa dini na asiye na maadili yoyote kwa kifupi msumbufu, ila ataishi kwa miaka mingi duniani

Je ungekuwa wewe ungechagua yupi kati ya hao wawili?!!

NAOMBA JIBU SERIOUSLY.
THANK YOU
 
Kweli mi na dhani
unatania.. hapa ni sawa
unauliza kwanini maiti haina
pumzi..
 
Sijaelewa mantiki ya swali lako maana halina uhalisia!!

We kama shida ni mtoto omba...ukimpata shukuru!!Malezi ndo yatamjenga au kumboa...
 
Sijaelewa mantiki ya swali lako maana halina uhalisia!!

We kama shida ni mtoto omba...ukimpata shukuru!!Malezi ndo yatamjenga au kumboa...

lizzy mamaaa chagua jibu moja tuuu
 
Habari

Naomba msaada juu ya HILI.

Eti mfano wewe umehangaika kupata mtoto muda mrefu sana na hatimaye.. mungu ameamua kukupa mtoto ila akakwambia uchague kati ya haya

1)Akupe mtoto mwema ambaye ni mchamungu na mtiifu ila ataishi kwa miaka ishirini tu atamchukua yaani atafariki.

2)Akupe mtoto mtukutu,asiyependa dini na asiye na maadili yoyote kwa kifupi msumbufu, ila ataishi kwa miaka mingi duniani

Je ungekuwa wewe ungechagua yupi kati ya hao wawili?!!

NAOMBA JIBU SERIOUSLY.
THANK YOU

Kutumia ikili yako vyema ni pamoja na kugundua kuwa si kila kitu kinafaa kujibiwa,ndiyo maana waliotangulia hakuna aliyejibu swali lako...hakuna mantiki kwenye hilo swali ndugu.
 
vitoto vya o'level utavijua tu kwa vihoja na viswali vya kipuuzi
 
Nenda shule wewe naona uko shift ya mchana na angalia mother kaacha kiasi chake kwenye moderm akirudi toka kazini akute imepungua utaipa pata.
 
mungu ameamua kukupa mtoto ila akakwambia uchague kati ya haya
hamna mungu wa hivyo, labda kwa waganga wa kienyeji na majini.
 
Huyu Mungu wa 'machaguo' anapatikana wapi? Nina mtaka sana ili tu-sort out katatizo kamoja kadogo.
Nina kisukari, nataka anipe option nyingine. Seriously
 
jamani kwanini msichague jibu moja kati ya mliyopewa....ni swali dogo tu la kutegwa akili, No wonder y watanzania wanafeli sana mitihani. unaulizwa kingine we una tengeneza swali au hoja zako binafsi, mkifeli visingizio vingi.

HAPO NI majibu mawili tu chagua na sio hoja binafsi. mweeh!!
 
hehehe hamna kitu hapa!
mkuu hiyo mia tano ya cafe unayoenda kuanzishia sredi bora kapigie supu ya utumbo tu upate vitamin C.
Suala la Mungu unatuuliza sisi bana?
 
Hivi mlango wa kuingilia mbiguni ukitokea duniani upo wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…