Swali kuhusu NSSF

Sangarara

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
13,104
Reaction score
5,659
Huko nyuma ilifikia hatua nilimuomba Mheshimiwa ZITTO kabwe apunguze speed yake kwenye namna alivyokuwa akiipigia chepuo NSSF kuwekeza kwenye miradi ya Kisiasa hasa umeme kwa sababu kwanza iliishaonekana kwamba hawajaonyesha prudence kwenye maeneo mengine walikowekeza kama Kiwira,General Tyre na maeneo mengine.

Mtu kama mimi, nilifikia hatua hiyo sababu niliona kuna hatari ya mafao yangu kuja kupotea sababu ya uwekezaji wa kisiasa unaofanywa na unaolazimishwa kufanywa kupitia mashirika ya hifadhi za jamii.

Leo, imekuja kubainika kwamba sheria ya mafao ya wafanyakazi imechakachuliwa, kwa msingi ambao ni wazi kabisa una nia ya kuyapatia mashirika haya liquidity ya kuspend kwenye hizo investments, Bila kwenda kwenye details zaidi ambazo zinaendelea kutolewa na watu mbali mbali, naomba nijielekeze kwenye swali la msingi.

Msingi wa Swali
Ukaribu wako na NSSF na serikali unajurikana nchi nzima, naomba uniaminishe japo mimi binafsi kwamba, haukuwa na clue yoyote ile ya kuyawezesha mashirika haya kifedha kwa kuwakandamiza wafanyakazi. Imani yangu ni kwamba kwa namna ulivyo na mahaba ya kuona mashirika haya yanashiriki kwenye uwekezaji ni lazima hii funding plan uiliielewa kabla.

AU. Ni wewe ndio uliye come up na huu mkakati?
 
Swali zuri, ila ni vyema likajibiwa na mhusika au hata kama na watu wengine basi itabidi hekima itumike ili msije mkaingiza na mambo yasiyohusika.
Napita tu na kila la kheri.

FEAR NOT.
 
Swali zuri sana_ila ingekuwa vema kama lingeelekezwa kwa wabunge wetu wote,..
 
mpaka 2015 umaarufu wa zitto kwishen kabisa. take heart broda. Sangara nakujua wewe ni CDM Damu kwahiyo uliyoandika ni mazito kama ulivyo mzito na wewe
 
hapa namtetea zitto..hawa majambazi wameleta hii sheria siku nyingi baada ya kauli ya zitto kuwatetea nssf...i don't see how zitto could be linked to this crime
 
Swali zuri sana_ila ingekuwa vema kama lingeelekezwa kwa wabunge wetu wote,..

Nadhani nimejitahidi kwa uwezo wangu wote kuonyesha ni kwa nini hili swali linapaswa kujibiwa na ZITTO.
 
hapa namtetea zitto..hawa majambazi wameleta hii sheria siku nyingi baada ya kauli ya zitto kuwatetea nssf...i don't see how zitto could be linked to this crime

Ukiangalia hoja yangu vizuri utagundua kwamba katika wabunge wote waliopo pale bungeni, about 350 of them, ni ZITTO pekee ndio mwenye network za kuweza kuliona hili kabla halijatimia.
 
mpaka 2015 umaarufu wa zitto kwishen kabisa. take heart broda. Sangara nakujua wewe ni CDM Damu kwahiyo uliyoandika ni mazito kama ulivyo mzito na wewe
Zitto bado ana nafasi kubwa sana ya kujirekebisha na akarudisha imani ya watu kwake.
 
Zitto bado ana nafasi kubwa sana ya kujirekebisha na akarudisha imani ya watu kwake.

Na hapa nimempatia nafasi adhimu ya kujirekebisha, sababu haya mambo yanazungumzwa uku mtaani. Jana hii hoja iliibuka sehemu sikuweza kuizima, ndo mana nataka majibu kutoka kwake mwenyewe.
 
mpaka 2015 umaarufu wa zitto kwishen kabisa. take heart broda. Sangara nakujua wewe ni CDM Damu kwahiyo uliyoandika ni mazito kama ulivyo mzito na wewe
Sio kwamba atakuwa Strong zaidi?
 
Ni kweli nakumbuka Zitto aliwahi kuhamasisha Mashirika ya NSSF na PPF kuwekeza kwenye uchumi wa ndani, badala ya wawekezaji kutoka nje. Sina hakika kama alijua au alifanya analysis.
Sidhani kama Zitto anafahamu kuwa NSSF inaelekea kufilisika kutokana na kujiwekeza kwenye majengo ya serikali pamoja na majengo ya kwake yenyewe!
Kama anafahamu basi yeye ni mmoja wa watakaofaidika na mkakati wa kuzuia fao la kujitoa uanachama!
Pia kama anafahamu, lile suala la udini kwenye hii taasisi muhimu la NSSF litakuwa na kaukweli kwa mbali, manake baada ya Dr. Dau kuteuliwa kuwa mkurugenzi ilifikia hatu kati ya nafasi 10 za kazi NSSF 8 lazima wawe watoto wa mamdogo.
 
Last edited by a moderator:
mm naona wabunge wote, kama kweli wako serious na kutetea wanyonge, wasiipitishe budget ya wizara ya kazi mpk sheria kandamizi irekebishwe
 
mm naona wabunge wote, kama kweli wako serious na kutetea wanyonge, wasiipitishe budget ya wizara ya kazi mpk sheria kandamizi irekebishwe

Ni sawa, wabunge wote wanawajibu wa kuhoji haya mambo, lakini wewe na mimi tunaelewa kwamba wabunge wa ccm hawawezi kuhoji haya mambo.

Pili, kuna baadhi ya mambo wabunge wanaweza kuyahoji kutokana na access waliyonayo ya information. Katika hili ZITTO ana access kubwa ya information kuliko hata Madam Speaker kutokana na interests ambazo amekwisha kuzidhihirisha kwetu kutokana na namna anavyokazania NSSF ipewe investment opportunities maeneo mbali mbali. Ndio maana mimi namuweka kwenye nafasi ya juu zaidi ya kuwajibika kuliko wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…