Swali kwa ma-specialist wa mambo ya UZAZI

queenkami

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2010
Posts
1,694
Reaction score
1,249
Heshima kwenu Wakuu.

1.Eti ni kweli kwamba mtoto akizaliwa premature wa miezi 7 anayo nafasi kubwa ya kusurvive kuliko premature wa miezi 8?
Kama jibu ni ndio nitafurahi kufafanuliwa ni kwa nini.

2.Nafahamu kwamba mtoto anapokua tumboni kuna wakati kichwa chake hugeukia kule chini anapotokea,sasa naomba kujua Je hicho kichwa kinapodondoka kutizama chini ni kitendo kinachofanyika taratibu kwa masiku Kama vile mshale wa saa unavyoenda taratibu kuelekea pale kwenye saa 12 au inatokea siku mama mjamzito Anasikia tu ghafla mtoto akiflip kichwa chini?

3.Je mama mjamzito ikitokea akalalia tumbo,atamkandamiza mtoto wake hadi afe?

natanguliza shukrani.
 
tarehe 19 au 20 januari 2012 uliuliza maswali humu nakumbuka nilikujibu . hujamaliza utafiti?!!

nikifika ntakujibu haya
 
tarehe 19 au 20 januari 2012 uliuliza maswali humu nakumbuka nilikujibu . hujamaliza utafiti?!!

nikifika ntakujibu haya

Ni kweli nakumbuka ulinisaidia sana kupata majibu wakati ule.
Maswali haya hayahusiani na yale ya mwanzo.
Nakusubiri kwa hamu ukifika unipe majibu my dear.
Thanks in advance
 
mimi ni mja mzito. inawezekana ikifika miezi nane na nusu kufanyiwa operation? maana mimi nitafanyiwa operation. je kunamadhara yoyote yale
 
miezi mingapi ndo mwisho wa kufanya mapenzi wakati kama ni mjamzito?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…