Swali kwa Mohamed Said, Kwanini majina ya ukoo maeneo ya Pwani yalikuwa?

Swali kwa Mohamed Said, Kwanini majina ya ukoo maeneo ya Pwani yalikuwa?

Airfryer

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2021
Posts
430
Reaction score
1,039
Pwani ya Dar es Salaam ambako watu walimpokea muarabu wengi wao majina ya ukoo hawataki kuyatumia na wengi hawayajui, Mfano kuna watu waliitwa Juma Tambaza na Tambaza ni jina la ukoo. lakini Wengine wote huwa siwaelewi.

Majina yetu ya ukoo yapo kabla ya mkoloni na dini, kwani tulikuwa na maisha yetu.
.
Mtu anaitwa Salum Mohamed Juma, Hivi hapa kuna jina la ukoo? Juma ni jina la ukoo?

Mtu anaitwa Mohamed Said, Hapa kuna jina la ukoo kweli?

Kila nikiwahoji watu wa Dar es Salaam wazawa kuwa mbona akina Tambaza ni koo au Makuburi ni koo, Wengine mnaiita Khadija Juma Jaffer, Jaffer ni jina la ukoo? Wengine wanajiita Abdallla Mohsin Issa, Issa ni jina la ukoo?

Ukiuliza koo zenu ni zipi hawazijui wala kuzitambua wanasema hata wao hawaelewi kilitokea nini

Kwanini maeneo ya Pwani watu walijigeuza majina yote mpaka la ukoo hawajulikani

Pwani ya mtwara na lindi kidogo watu wana majina ya ukoo

Mfano Musa Adam Chinguile, Chinguile ni jina la ukoo maeneo ya mtwara huko

Mohamed ally Nanyecha, Nanyecha ni jina la ukoo maeneo ya mtwara na lindi

Sasa hawa wazee akina Mohamed Said, Koo zao ni zipi?

Lazima historia yetu ilindwe na iandikwe upya, Haiwezekani mtu kama Mohamed Said asiwe na jina la ukoo na Wengine wengi ya Pwani ya Dar es Salaam wakati dini zilitukuta tuna majina na koo zetu.

Tulinde historia yetu kama Mohamed Said anavyopigania, Na hili lazima tuliseme kuhusu majina ya koo maeneo ya Pwani kutojulikana yameenda wapi.
 
Unataka ujibiwe nini mkuu zaidi ya matokeo ya utumwa wa kidini/kitamaduni.
 
Unataka ujibiwe nini mkuu zaidi ya matokeo ya utumwa wa kidini/kitamaduni...
Kwa hiyo Mohamed Said anavyopigania historia ya uhuru ni muongo maana Yeye mwenyewe anajiita Mohamed Said, Sasa Said ni jina la ukoo?

Kikwete ni jina la ukoo na la asili ya waafrika, wanaojiita Abdalla Salum Hamza mbona ukiwauliza jina la ukoo hawalifahamu na wao hawajui kilitokea nini? Hamza ni jina la ukoo

Hii historia akina Mohamed Said lazima waiseemee na iandikwe upya kwa uhalisia hasa majina ya hizi koo

Yawezekana Mzee Mohamed Said analalamika sana kwenye historia ya uhuru na vita vya majimaji lakini anashindwa kutambua maeneo ya Pwani yalikumbwa na mzimu gani mpaka kupelekea majina ya koo kwa kundi kubwa la watu kutoeleweka na kupotea

Koo nyingi hasa za Pwani na bara zina majina yake ya kiafrika na unique

Mfano Tambaza, Makuburi, Dinyecha, Mwakifuna, Mwafilombe, Ngonyani, Mbawala,
 
Air...
Majina ya ukoo naamini unakusudia majina ya asili.
Nkuwekea majina yangu naamini utatambua na nitakuwa nimejibu swali lako.

Mimi naitwa Mohamed Said Salum Abdallah Mwekapopo Samitungo Muyukuwa,
Nimekwenda nyuma vizazi saba.

Haya majina ni ya wale tuliozaliwa Tanganyika na Belgium Congo.

Katika ukoo wangu wapo waliozaliwa Tanganyika na wakapewa majina ya Kimanyema mfano wa Numbi, Mwamba, Mwekapopo nk. na niko mimi iliyepewa jina la Mohamed.

Huyu Mohamed ni Sheikh Muhammad Mvamila babu yangu mzaa mama.

Na huko Belgian Congo wapo waliopewa huko majina ya Farjallah na wakaja kuzaliwa watoto Tanganyika wakarithishwa majina hayo.
 
sabauna wapemba hujiona waarabu hata kama ni weusi na kipilipili
Mdukuzi,
Nitawasemea Wamanyema kwani ndiyo kabila yangu.
Mmanyema kujiona kuwa ni Muarabu hili ndiyo leo nalisikia kutoka kwako.

Ila ninachojua mimi Wamanyema wanawastahi sana Waarabu kwa kuwa (na hili nimelisikia Wamanyema wakisema) ni kabila ya Mtume Muhammad SAW na Waarabu ndiyo waliowaletea Uislam.

Wamanyema ni kabila la Waislam watupu.
 
Air...
Majina ya ukoo naamini unakusudia majina ya asili.
Nkuwekea majina yangu naamini utatambua na nitakuwa nimejibu swali lako.

Mimi naitwa Mohamed Said Salum Abdallah Mwekapopo Samitungo Muyukuwa,
Nimekwenda nyuma vizazi saba.

Haya majina ni ya wale tuliozaliwa Tanganyika na Belgium Congo.

Katika ukoo wangu wapo waliozaliwa Tanganyika na wakapewa majina ya Kimanyema mfano wa Numbi, Mwamba, Mwekapopo nk. na niko mimi iliyepewa jina la Mohamed.

Huyu Mohamed ni Sheikh Muhammad Mvamila babu yangu mzaa mama.

Na huko Belgian Congo wapo waliopewa huko majina ya Farjallah na wakaja kuzaliwa watoto Tanganyika wakarithishwa majina hayo.
Hapo sasa sawa na Hongera Mzee

Mimi nitakuita Mohamed Said Mwekapopo

Nimekukubali sana kwa kuwa na jina la koo lakini kwanini Wengine hawayajui kabisa majina yao ya koo na ni watu wazima na hata ukiwauliza ilikuwaje hawaelewi ndio swali langu
 
Unaweza kuniita upendavyo ila utakuwa umepoteza utambulisho wangu.
 
Godo, Mtimbwiliko, Simba, Singano, Mwanambaya n.k ni majina yetu ya ukoo watu wa Pwani
 
Back
Top Bottom