Swali kwa Mwakyembe: Ina maana alilidanganya Taifa juu ya Richmond? Ukweli upi atauleta ulio kweli?

Tuna watu wengi wanaijua sana biblia lakini ni watenda dhambi wakubwa.

Mwakyembe ni kama askari aliyepewa silaha nzuri kwaajili ya kulinda jamii yake lakini akageuka kuwa jambazi, akaitumia silaha ile ile kuiangamiza jamii yake. Huyu anakuwa jambazi hatari kuliko jambazi asiyekuwa na mafunzo ya kutumia silaha.

Nikuambie kitu!!! Kama unauwezo wa kumfikia Mwakyembe na akawa na muda wa kutoa somo juu ya haki asilia, fanya hivyo. Anajua kila nadharia hata Lisu unayemuamini kafundishwa na huyu.
 
Hayo ni mabunio yako, nenda kayahakiki kwa kufanya uchunguzi. Utakuja kutupa ukweli uliouona unaothibitisha mabunio yako. Ila siwezi kuamini haya kwa sasa.
 
Ndio maana mwakyembe amesema alivyosema kama wanabisha hoja irudishwe mezani waone kama manywele hatanyea ndoo
Kwa hiyo mahakama ya mafisadi ni ya kinanani? Kwanini asipeleke huo ukweli huko? Kilichomfanya kuficha ukweli mwingine ni nini? Nani alikuwa analindwa hapo? Wote tunajua muhusika mkuu alikuwa nani, je anataka kumlipua sasa hivi kwa sababu hayupo madarakani? Je unajua tukiamua kuchuja watu safi ndani ya CCM hakuna atajaye pona? Je unafahamu ishu za mzee wa mabarabara zinajulikana sana ila watu wamefumba macho tu? Unajua ishue za Mwaki na mabehewa?
 
Haya ni mabunio. Njoo na utafiti wa kuyathibitisha.
 
Usitujazie server bure.Mwakyembe kasema kama mnaona Lowasa alionewa au kwanamna moja au nyingine makosa yalifanyika pelekeni hoja bungeni ili lile sakati lirudiwe kujadiliea bungeni
Hahahaha kwahiyo ninyi wabunge wa ccm hamna uchungu na ufisadi ktk nchi hii hadi Chadema pekee wanaoweza kupeleka hoja tena ndani ya bunge?!!!!
 
Hayo ni mabunio yako, nenda kayahakiki kwa kufanya uchunguzi. Utakuja kutupa ukweli uliouona unaothibitisha mabunio yako. Ila siwezi kuamini haya kwa sasa.

Wengi wanaigiza upofu!!!
Sio mbaya kama ukiamua kuwa kipofu!
Samahani kada!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…