SWALI: Kwa nini siku hizi kuna baadhi ya siku mwezi unaonekana mchana?

SWALI: Kwa nini siku hizi kuna baadhi ya siku mwezi unaonekana mchana?

torvic

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2016
Posts
3,978
Reaction score
9,841
Habari zenu waungwana,

Najua hili swali limekaa kitoto lakini ukijiuliza hata wewe nadhani utafikiria kidogo haswa kama unaufahamu kidogo na mambo ya anga, kama wote tunavyofahamu jua huangaza mchana linachomoza mashariki linazama magharibi na mwezi nao uangaza usiku, kisomi hapo tunasema dunia ikijizungusha tunapata usiku na mchana. (sijui ndio ivoo)

Sasa mimi mshangao wangu na swali langu lianakuja pale napouona mwezi ukioneka kama majira saa 10 had saa 11 za jioni na ulitakia kuonakana usiku? kuna nini labda kinatokea mpaka tunauona muda huo na sio usiku kama inavyotakiwa.

Hapa naona kwa wenye elimu ya astronomy au believes zozote ningependa kujua inakuaje kuaje hapo?
 
Kweli swali la kitoto, mwezi umekuwa ukionekana muda huo tangu enzi na enzi. Mwezi unakuwa katika mzunguko wake wa kawaida, wapo wanao uona wakiwa gizani na wengine ikiwa bado ni jioni.
Kumbuka kuwa mwezi pia huchomoza usiku sana unapokaribia kuingia gizani, pale unapochomoza saa saba usiku basi utaonekana mchana kutwa. Tatizo ni kwamba mwanga wa jua ni mkali kwa hiyo mwezi hauonekani kirahisi.
 
jamaa alitaka kusema pia nyota huwa hazipo ikifika usiku ndio zinatokea huko zilipokuwa zimejificha!bila kufaham kwa hivi vitu vipo tu muda wote toka dunia iletwe duniani
 
Tangu nikiwa sijaenda hata chekechea nilikuwa nauona mwezi mchana, usiku, asubuhi na jioni
 
Back
Top Bottom