Swali kwa serikali: Hawa Wachina walioweka madubwi kila kona Tanzania nao ni wawekezaji?

Swali kwa serikali: Hawa Wachina walioweka madubwi kila kona Tanzania nao ni wawekezaji?

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
1708990819609.jpg

Sijasomea uchumi ila kwa hesabu za haraka haraka tu mchina akizunguka mitaa 5 tu ya Dar es salaam anakusanya mpaka sh. Milioni 100 za Watanzania kupitia madubwi au mabonanza wengine huyaita.

Mtaa mmoja una slots machines 20-50.
Mchina anaweka sarafu za sh. 200, ambazo zinakuwa sarafu 300 sawa na sh.60000
Kesho saa tatu mpaka saa tano asubuhi anakusanya sh. Laki 3 mpaka laki 5 au zaidi.
Kati ya madubwi 100, ni dubwi 1-2 ndio hupata hasara , huku madubwi 98-99 hupata mavuno manono kutoka kwa Watanzania waliokosa ulinzi wa kiuchumi kutoka kwa serikali yao.

Haya madubwi yamekuwa kama kilevi, watu wenye kipato kidogo a.k.a maskini au wanyonge ndio wahanga wakubwa , wakipata kidogo wanakwenda kujaribu bahati nasibu wanarudi mikono mitupu.

Uchumi wa nchi unamegwa na watu kutoka Uchina.
Serikali mko wapi?
Watumishi wa bodi ya Bahati nasibu hawakagui hizi mashine za unyonyaji, na hawana vifaa vya kukagulia hizi mashine kama zinazingatia ubora wa kimataifa. Wachina wanaziseti wanajipa mpaka 98%, Watanzania wanapewa 2%.

Mabilioni ya fedha za Kitanzania yanachotwa na Wachina huku serikali ikijisahau na kidogo.
Nimefanya utafiti wa kutosha kuhusu haya madubwi ya Wachina.
Watu wa bodi ya Bahati nasibu miguu juu, wakipewa hongo kidogo wanatulia.

Uchina haya ma6dubwi hayaruhusiwi. Na mtu binafsi akichezesha haya madubwi anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha au kifo kabisa.
Hivi serikali hii imelala kiasi gani?
Ikitokea kadhia mahali na ikaonekana mitandaoni hapo ndipo viongozi wanaamka na kutoa kauli.
Inafika wakati unawaza mpaka unasema Mungu ametunyima akili Watanzania.

Tukio lolote likionekana mtandaoni hapo ndipo unaona makali ya viongozi.
 
Back
Top Bottom