Utaratibu wa kutangaza kwamba rais ana matatizo ya kiakili/kimwili na kwamba hataweza kuendelea kuongoza unahusisa mihimili yote mitatu, ambapo kunakuwa na azimio la baraza la mawaziri kwenda kwa jaji mkuu kumwomba athibitishe rais hawezi kuongoza, jaji mkuu atateua jopo la madaktari 10 ambao watamchunguza na kumshauri juu ya afya ya rais na jaji mkuu atawasilisha mapendekezo yake kwa spika wa bunge (Ibara ya 37(2).
Mengineyo ni kama yanafanana. Panapopatikana sababu ya kumshitaki rais mf. Anapokiuka katiba nk, atashitakiwa na bunge kwa mujibu wa Ibara ya 46A ya katiba. Kwa makosa mengineyo rais anayo kinga dhidi ya mashtaka na madai.