Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Swali kwa Wanaotaka Kura ya Siri: Hoja kubwa inayotolewa na wale wanaotaka kura ya siri kwenye Bunge la Katiba ni kuwa hawataki watu wajioneshe wanapigia kura wapi kwa sababu inawapa shinikizo kufuata maelekezo ya kichama na pia inaweza ikaleta uhasama dhidi yao. Wanasema kura ya wazi siyo ya kidemokrasia na kuwa watu wataogopa kupiga kura kwani wataonekana kura yao imepigwa vipi; ni bora wapige kura ya siri ili tuone matokeo tu.
Inawezekana vipi kutaka kura za siri lakini wakati huo huo kutaka mijadala ya wazi hata ile ambayo ni ya Kamati?
Sasa swali langu ni je wanaotaka kura ya siri wako tayari pia kukubali baadhi ya vikao vya Bunge la Katiba kuwa vya siri kwa sababu hizo hizo? Ili kwamba wabunge wawe huru kujadiliana na kuchukua maamuzi mbalimbali bila kujionesha mbele ya wapiga kura? Kwamba baadhi ya vikao vya kamati vifanyike kwa siri ili kulinda uhuru wa wachangiaji wake?