SWALI KWA WATU WA MANUNUZI SERIKALINI.

SWALI KWA WATU WA MANUNUZI SERIKALINI.

Munjombe

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2018
Posts
2,107
Reaction score
2,985
Kuna mdau anauliza ikitokea mkandarasi alisaini mkataba wa kujenga kilomita 50 za lami labda kutoka Njombe kwenda Ludewa baada ya kufika site anaona mbona kuna njia ya mkato naweza kupunguza kilometa kutoka 50 hadi 48 au 49 na nitaserve almost 3bil.Je hapo serikali itakuwa imelipa kilomita 49 au 50 na ikiwa kilomita zimepungua kwa kuchepusha barabara eneo tofauti na eneo la mradi alilokabidhiwa ni sawa kubaki na mkataba wa awali wa kilomita 50 au kunahitajika adjustment kwenye mkataba?Na ikitokea mkandarasi na watumishi wa serikali wameificha serikali uhalisia wa kupungua kwa hizo kilomita haliwezi kuwa ni kukiuka maadili?
 
Kiongozi kwanza kabisa utekelezaji wa mradi wa ujenzi hufuata, BOQ ambayo ndiyo inayo onyesha details zote za kazi zinazotakiwa kufanywa kwenye ujenzi wa hiyo barabara, pia malipo ya kazi ya ujenzi hufanywa baada ya kuwasilisha certificate ya kiasi cha kazi kilichofanyika hivyo kama kazi itafanyika ya km 48 maana yake malipo yatakayofanyika yatakuwa ya km 48, na kama itaonekana barabara inaweza kuchepushwa na kupunguzwa basi hapo lazima kipengere hicho kiongezewe kwenye mkataba mkuu na kieleze bayana juu ya mabadiliko yanayofanyika hapa lazima pande mbili zikubaliane, lakini pia wakati wote wa utekelezaji wa mkataba kuna mtu ambaye anakuwa ndiyo msimamizi wa mradi ili kuhakikisha utekelezaji wa mkataba unafuatwa kwa usahihi kama mkataba ulivyosainiwa.
 
Back
Top Bottom