SWALI KWA WIZARA :Nini UMUHIMU WA KWENDA SHULE?

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2010
Posts
7,264
Reaction score
678
WanaJamvi mimi nina maswali yangu kwa Wizara ya elimu

Nina watoto wangu bado wanaendelea kusoma lakini mimi nimetumia nguvu nyingi kusoma mpaka nimefikia hapa nilipo kwa elimu yangu inanitosha kuisha katika maisha haya, sasa nina mpango wa kuwaachisha watoto wangu shule/chuo maana siku hizi vyeti mtu unapewa hata kama hujaenda shule. Nataka kufanya uamuzi huu maana inauma na kusikitisha saana kuona watoto wangu wanaenda shule/chuo wakati wengine wanapewa vyeti na mavyeti


Maswali kwa Wizara ya Elimu

1. Taifa linaenda wapi kama kula mtu atajigawia cheti na kusema kasoma?

2. Je kuna haja gani ya watu/watoto wangu kwenda shule/chuo?

3 Kuna haja gani ya kuanzisha vyuo kama UDSM or UDOM etc?

4. Kwanni watu wanapewa vyeti na kuvitumia wakati hawajaenda dalasani? Wizara na idara zake (TCU) wamelala?

5. Kwanini watu wanatumia vyeti vyao kuwazalau walioingia darasani?


6. Je madarasa tuyageuze majumba ya makumbusho??

WanaJF msaada wenu
 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…