Swali: Kwanini Mbuni Habuni?

Swali: Kwanini Mbuni Habuni?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
ostrich-head-in-sand.jpg

Ya’raabi nipe kauli, niseme hili na lile,
Kauli isiyo kali, isiwe kama ya yule,
Niseme lililo kweli, la mbuni hawa na wale,
Mbuni kichwa mchangani, kwanini mbuni habuni?

Mbuni wana ile hali, hali yao ile ile,
Ukiuliza maswali, jawabu ni lile lile,
Watakukata kauli, ukajikuta mpole,
Mbuni kichwa mchangani, kwanini mbuni habuni?

Mnyama yule mkali, kawafuata mbuni kule,
Na meno yake hatari, kaingia hadi mle,
Akagenda nyalinyali, wasishtuke mbuni wale,
Mbuni kichwa mchangani, kwanini mbuni habuni?

Mbuni wakaona zali, wakajifiche kule,
Wakajibanza kwa mbali, wakimkimbia yule,
Wakatafuta mahali, asije yule awale,
Mbuni kichwa mchangani, kwanini mbuni habuni?

Walipopata mahali, wakafanya vile vile,
Mchangani wakisali, wakajichomeka pale,
Hawakuuficha mwili, eti yule asiwale,
Mbuni kichwa mchangani, kwanini mbuni habuni?

Swali langu ndilo hili, ninawauliza wale,
Mbuni wanazo akili, au akili zao ni zile,
Za kutokuficha mwili, kisa kichwa kiko kule,
Mbuni kichwa mchangani, kwanini mbuni habuni?

Nimeuliza hili, nazifunga beti zile,
Nafunga zangu kauli, naendelea na yale,
Msiniite katili, kwa kukumbushia lile,
Mbuni kichwa mchangani, kwanini mbuni habuni?

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
Nje ya Jiji la Detroit, MI (USA).
 
Natakiwa nimjue mbuni ni nani kwa huu muktadha ili nijue kwa nini hafirii? Je mbuni amekaririshwa kutokufikiri ? Au anaiona hali lakini ameamua makusudi kabisaa kufichwa kichwa sehemu muhimu ktk kufikiri?
Wanaomjua mbuni karibuni.
 
Hata ukiuliza maswali,utajibiwa vilevile!

Mbuni mbunifu alikufa awali,
Walimkata kwa kisu
wakala na kachumbali!

mbuni lake tifu,liliwashinda mahodari
 
Mbuni
Natakiwa nimjue mbuni ni nani kwa huu muktadha ili nijue kwa nini hafirii? Je mbuni amekaririshwa kutokufikiri ? Au anaiona hali lakini ameamua makusudi kabisaa kufichwa kichwa sehemu muhimu ktk kufikiri?
Wanaomjua mbuni karibuni.
mbuni wengi makatili,kura tuliwapatia.
maneno yalobatili,ndicho walotupatia.
leo hii utakiri,wengi leo twajutia.
mbuni kichwa mchangani,kwanini mbuni habuni?
 
barabara wakipita,mtutu kutushikia.
kura nitawapatia,kauli mbiu sikia.
Hapa kazi tupatia,mbuni wanatusikia.
Mbuni kichwa mchangani,kwanini mbuni habuni?
 
barabara wakipita,mtutu kutushikia.
kura nitawapatia,kauli mbiu sikia.
Hapa kazi tupatia,mbuni wanatusikia.
Mbuni kichwa mchangani,kwanini mbuni habuni?
Mbuni kala yamini, katu asibuni,
Kashindwa sabuni kubuni.

Kuondoa kunguni mwilini,
Mbuni kiwiliwili kichwa chini mchangani,

Mbuni katuweka mtunguni, kama samaki wa ziwani.

Hatusemi hatuhemi, mwili kunguni sheheni.

Mbuni abuni sabuni, tuondoe kunguni mwilini.

Ishirini tatu zi karibuni, kunguni wafika shingoni.

Mgongoni si gogoni, sabuni katu habuni!

Mambo yasiwe mengi, mengi yasiwe mambo
 
brother laiti kama serikali ingelikua inazingatia uwezo wa watu basi naamin kabisa sisi tungekua kwenye nafasi kubwa sana lakini cha ajabu.

shamba laungua moto,vitalu vyateketea.
kitalu chngu kidogo,ndipo nilipotokea.
ngoma yetu baikoko,Tanga naiongelea.
japo shubiri ni tamu,ahueni tulipata.

mji ule wa mapenzi,mji mashuhuri sana.
tunapokumbuka enzi,Tanga tunalia sana.
viwanda vilisheheni,saruji nguo na chuma.
japo shubiri ni tamu,ahueni tulipata.
 
Back
Top Bottom