MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
Taifa la Kenya lina jamii mchanganyiko.
Ila moja ya jamii ambayo ni ya kipekee sana ni Wasomali ambao kiuhalisi walijikuta wako Kenya kutokana na sababu za kikoloni. Ila baada ya Kenya kupata Uhuru 1963, Wasomali waliokuwa wanakaa maeneo ya Kaskazini walianzisha mkakati wa kijeshi kujitoa Kenya ili kujiunga na Somalia.
Vita hiyo iliitwa, SHIFTA (The Shifta War), ambayo ilidumu kwa takribani miaka minne na kusababisha vifo vya watu 10,000. Huku waasi wakiwa wanaungwa mkono na serikali ya Somalia ambayo iliwapa msaada wa silaha na vitu vingine hadi kupelekea mahusiano ya kidiplomasia baina ya Kenya na Somalia kuharibika.
Mwaka 1967, chini ya OAU, Raisi Kaunda alifanikiwa kusuluhisha huo mgogoro kule Arusha. Japo Kenya kujiponya iliamua kusaini makubaliano ya ulinzi na serikali ya Ethiopia ambayo nayo ilikuwa na tatizo la namna hii na Somali kule Ogaden. Matatizo yalikuja kutulia baada ya Serikali ya Somalia kuanguka na kupoteza mwelekeo mwaka 1975 baada ya kupigwa vibaya na Ethiopia kwenye, vita vya Ogaden (The Ogaden War).
Jambo jingine ambalo Raisi MOI alilifanya ni kuhakikisha Wasomalia wanaingizwa kwenye nafasi mbalimbali nchini Kenya, ili wawe raia ili wasisumbue tena. Baada ya kuona anachukiwa na WAKIKUYU na WAJALUO, Raisi MOI alijaza Wasomali kwenye vyombo vya ulinzi na usalama vya Kenya. Hawa wasomali ndiyo walimsaidia akwepe majaribio kadha wa kadha ya kuuwawa na kupinduliwa. Naona hii mbinu RUTTO naye anaitumia, japo sidhani kama itafanya kazi.
JAMBO AMBALO NAJIULIZA SANA NI HILI: Siku Somalia imetulia na kuwa taifa liloungana kama zamani, na ukichukulia jinsi Wasomali wanavyojivunia Usomali wao, popote pale walipo duniani, Kenya itakuwa na hali gani kiusalama ukizingatia Wasomali wameweza kufika kwenye ngazi kubwa za usalama wa nchi hiyo kama DIRECTOR OF INTELLIGENCE and CHIEF OF DEFENCE FORCES ???
Wanaweza wasiwavamie WAKENYA kama zamani, lakini kutokana na hali ya kuisalama nchini KENYA, hasahasa mvutano na chuki za kikabila wanaweza kujikuta wameitawala Kenya kimzahamzaha. Mbali na suala la kiusalama, Wasomali ni jamii yenye watu ambao wana hulka ya kujituma sana, hivyo wameshikilia biashara kubwa nchini Kenya. Ukienda hata Afrika Kusini, biashara za wasomali ziko moto sana.
=========================
MIFANO MICHACHE YA KIHISTORIA
1. USSR NA WAYAHUDI
Jambo kama hili liliwahi kuikuta Urusi miaka ya 1950's-1980's, ambapo sehemu kubwa ya jamii ya Kiyahudi ilikuwa inaishi Urusi. Wakati wa mapinduzi ya mwaka 1917, wayahudi wengi walikuwa mstari wa mbele hivyo wakaingizwa kwenye taasisi za ulinzi na usalama za USSR, kama NKVD/GRU/INO/OGPU/MGB/KGB na The RED ARMY.
Walipambana vita ya pili vya dunia kama wanajeshi wa Warusi, lakini mwaka 1948 wakati taifa la Israeli limeundwa na UMOJA WA MATAIFA mambo yalibadilika ghafla. Ikumbukwe Raisi Joseph Stalin alisaidia sana taifa la Israel kuundwa na yeye ndiye aliwapa silaha za kupambana na waarabu mwaka 1948 na kushinda, akitegemea kwamba Israeli litakuwa taifa la kikomunisti chini ya ushawishi wa USSR.
Bahati mbaya WAYAHUDI wa Marekani waliokuwa matajiri wakubwa walifanikiwa kuwavuta wenzao kutamani aina ile ya maisha hivyo wakahamia kwenye kambi ya Marekani na kugeuka maadui wa Urusi. Jambo ambalo lilihatarisha mno usalama wa USSR kwasababu Wayahudi wengi walishavifahamu vyombo vya usalama vya Urusi na walikuwa na watu wao ndani ya mifumo ya Urusi.
Warusi hawawezi kusema lakini, Israeli ilihusika mno kuhujumu USSR.
2. UGANDA NA WATUTSI
Leo hii Waganda wanatunishiwa misuli sana na Rwanda kwasababu, watawala wa Rwanda walishawahi kuwa na nafasi nyeti mno ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama vya Uganda. Sambamba na hilo, jamii ya Wanyankole ambayo ndiyo inatawala Uganda, kiasilia ilikuwa ni jamii ya ufalme wa Bunyoro Kitara ambao ulikuwa ni himaya ya Kitutsi.
Raisi Kagame kajaza majasusi wengi Uganda, hadi kupelekea Uganda kushindwa vita kizembe na nchi ya Rwanda kule Kisangani kwasababu waganda walizungukana. Wengine walikuwa kwa Museveni na wengine kwa Raisi Kagame. Kama serikali ya Rwanda chini ya Hyabarimana isingeanguka sidhani kama Watutsi wangetamani kurudi Rwanda, na wangeamua kuwa waganda kabisa.
3. ZAIRE NA WATUTSI
Huu ni mfano halisi kabisa ambao mpaka sasa unaishi. Jamii ya Banyamulenge ya DRC ni Watutsi ambao walienda DRC mnamo karne ya 19. Kipindi chote cha utawala wa Mobutu Sese Seko hawakuwahi kuleta changamoto sana, lakini matitizo yalianza pale ambapo ambapo Watutsi walifanikiwa kutawala Rwanda mwaka 1994.
Raisi Kagame akaanzisha ETHO-NATIONALISM ambayo iliiathiri Zaira kwa sehemu kubwa. Banyamulenge wakaanza kuamini kwamba wanaweza kutengeneza nchi yao, hata kujiunga na Rwanda. Bahati mbaya sana, Mobuthu alikuwa na ukaribu mno na serikali ya Hyabarimana ambayo ilikuwa ina ukaribu na serikali ya Ufaransa ambayo ilipingana na Watutsi ambao waliungwa mkono na Uingereza na Marekani.
Wakimbizi wengi wa kihutu walikimbilia Zaire na kuanza kujipanga kurudi Rwanda chini ya msaada wa Mobuthu, ambaye kwa wakati huo alikuwa ashaachwa na mabwana wake wa Ufaransa, Ubelgiji na Marekani kwasababu COLD WAR ilikuwa imeshaisha. Mwaka 1997, Rwanda ilivamia Zaire chini ya msaada wa Uganda na ushawishi wa kidiplomasia wa Raisi Nyerere na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa mno.
Lakini kabla ya uvamizi, Rwanda ilihakikisha inazorotesha mfumo mzima wa usalama wa Zaire. Ilitumia Banyamulenge waliokuwepo ndani ya vyombo vya ulinzi, na kuhonga wanajeshi na viongozi wengine ambao walikuwa wapenda rushwa. Sambamba na hilo, Zaire ilikuwa kama Kenya tu, UKABILA MKUBWA.
Rwanda walifanya hujuma kubwa mno kwa Zaire, hadi kuhakikisha kwamba siku wanavamia Zaire ambayo ilikuwa na jeshi kubwa lenye vifaa vingi zaidi, haliwezi kufanya chochote. Radar System ilizimwa, vifaa vingi vya kijeshi vilikutwa havifanyi kazi ghafla. Ndiyo yakatokea yaliyotokea na mpaka leo, DRC inachezewa na Rwanda na Uganda watakavyo.
4. MAREKANI NA JAMII ZA WAJAPANI NA WAJERUMANI
Kabla ya uvamizi wa Pear Harbour 1941, kuifanya Marekani iingine kwenye VITA VYA PILI VYA DUNIA, Marekani ilikuwa na idadi kubwa ya Wajapani na Wajerumani ambao walikuwa sehemu mbalimbali ndani ya nchi ile. Serikali za kifashisti za Ujerumani na Italia ziliamua kutumia mbinu za kutafuta majasusi ambao wangefanya uzandiki dhidi ya Marekani endapo ingeingia vitani.
Majasusi wa Ujerumani walifanya majaribio kadhaa kama OPERATION PISTORIOUS, ili kulipua miundombinu ya kiuchumi ya Marekani. Hili halikufanikiwa kwasababu baadhi ya majasusi walienda kujisalimisha kwa shirika la kijasusi la Marekani (FBI) hivyo kuwataja wengine waliokiwa wanapanga mipango hivyo.
Baada ya Marekani kufahamu kwamba Wajerumani (German Americans) ni wengi na isingewapata kirahisi, iliamua kusaini makubaliano ya siri na shetani (Devil's Bargain), ambapo mashirika ya kijasusi ya Marekani, FBI na OSS yalianza kushirikiana genge la CICILIAN MAFIA ambao walikuwa ndiyo wanaendesha mitandao mikubwa ya kihalifu nchini humo.
Mafioso kwasababu walikuwa wanazifahamu njia zote za magendo zote duniani, hasa kule Ulaya, waliisaidia Marekani kuua na kukamata maelfu ya majasusi wa Ujerumani. Ikumbukwe, The MAFIA walikuwa na ugomvi mkubwa na Serikali ya Benitho Mussolini hivyo waliwasaidia mno Wamarekani ambao hawakuingilia wala kugusa kabisa biashara za MAFIA.
Upande wa wajapani, Raisi Roosevelt aliamua kutengeneza THE CONCENTRATION CAMP, ambapo aliwafungia Wamarekani zaidi ya 120,000 wenye asili ya Kijapani kwa AMRI YA RAISI (EXECUTIVE ORDER). Wajapani wengi walionewa ila wengi waliokuwa na nia mbaya walidhibitiwa, ukizingatia Wamarekani ni binadamu ambao huwa hawana mzaha linapokuja suala zima la usalama wao.
========================
Mifano iko mingi sana ambayo siwezi kuitaja, kama ambavyo UCHINA ameweza kuwadhibiti UIGHURS ambao wana undugu wa karibu mno na Afghanistan na Turkic Muslims, waliotaka kujitoa kwenye jamhuri ya China.
Mwisho wa siku, bila ubaguzi wowote ule na chuki dhidi ya jamii fulani, Serikali za Kenya na Tanzania inabidi zijipange sana, maana lolote lile linaweza kutokea kwasababu jamii zetu ni Heterogenous. Mfano, hapa Tanzania kuna a considerable population of Tutsis, Hutus, Somalis, Indians and Arabs, hivyo aidha tujipange kama Afrika Kusini, Marekani, Uchina au tuishie kuwa kama Zaire na USSR.
Muwe na siku njema, ndugu zangu!