.Uzushi hauwezi kuwa muhimu.
Kutamani kunachuja haraka, vinavyotamaniwa mara nyingi vikikosekana ndio basi tena, tamaa haivumilii, tamaa haijali wala tamaa haina huruma. Mapenzi on the other hand kama yapo ya kweli utafaidi maana hata pale utakapokua una mapungufu mwenzio anaweza akayavumilia, ukimhitaji atakuwepo, ukianguka atakusaidia uinuke tena n.k
Sasa chagua mwenyewe hapo kipi kina nguvu.
.hivi unaweza linganisha tamaa na upendo kweli?
.Kupenda ni moto wa mkaa wa mti wa mgunga. Ni moto uwakao taratibu hivyo kuendelea kuwaka kwa muda mrefu sana lakini tamaa ni moto wa kifuu
.
What are the components of tamaa. Sura/mwonekano wa kuvutia or valuable material things? For what i guess (not sure) tamaa ndio inaanza na upendo ni baada ya tamaa kuota mizizi. Inawezekana kumpenda mtu ambaye hajakuvutia?
ofcourse unaweza kumtamani yule dada kwa maumbile yake, lakini simpendi, pia naweza kumpenda mke wangu ingawa sasa kapata ajali na umbo lake halipendezi ila bado nampenda, au ingawa physically simtamani ila nampendea character yake.Hivi unaweza kupenda bila kutamani kweli au Unaweza tamani bila kupenda?
Nijuavyo mimi vinavyo tamaniwa na vinavyopendwa vyote ni vizuri so what's the difference? Tofauti inakuja kuwa kwenye Upendo tamaa inadumu na kuendelea i think.
unaweza ukapenda na kutamani pia ila kutamani sio kupenda, kupenda ni zaidi ya kitu unachopata (au hamu uliyonayo) nikimaanisha kwamba ukipenda hata hicho ulichotamani mwanzo kikiondoka uwezekano mkubwa bado utaendelea kupenda tofauti na tamaa (ukikidhi haja yako tamaa inakwisha) yaani kama ukishakula mua unavyotupa lile ganda (utamu umekwisha !)Mi nauliza, unajuaje kama umependa au umetamani? Kuna mtu sijui nampenda, sijui namtani! Msaaaada plzzzz.
unaweza ukapenda na kutamani pia ila kutamani sio kupenda, kupenda ni zaidi ya kitu unachopata (au hamu uliyonayo) nikimaanisha kwamba ukipenda hata hicho ulichotamani mwanzo kikiondoka uwezekano mkubwa bado utaendelea kupenda tofauti na tamaa (ukikidhi haja yako tamaa inakwisha) yaani kama ukishakula mua unavyotupa lile ganda (utamu umekwisha !)
Nakutamani sijakuona siku nyingi natamani kusikia story zako natamani company yako tukiangalia movies, natamani kusikia kicheko chako na tabasamu lako..., lakini nakupenda kwa roho moja sitaacha kukupenda kamwe hata pale ukibadilisha mood yako ukaacha kutabasamu, kunipa company n.k.ahsante ila bado sijaelewa, kutamani ni nini na kupenda ni nini?
Nakutamani sijakuona siku nyingi natamani kusikia story zako natamani company yako tukiangalia movies, natamani kusikia kicheko chako na tabasamu lako..., lakini nakupenda kwa roho moja sitaacha kukupenda kamwe hata pale ukibadilisha mood yako ukaacha kutabasamu, kunipa company n.k.
hamu, kiu, shauku, curiosity n.k. naweza nikawa natamani company ya msichana ambayo kwenye bar yoyote ya karibu nitakidhi hamu yangu.., ila upendo kama ni kwa Hus basi Asha au Mwajuma hawawezi nitimizia..., and don't get me wrong huenda tamaa yangu ni ya kumpata Asha pekee basi hadi siku takapompata Asha tamaa haitaisha na huenda ninatamani kile alichonacho Asha hivyo mara kwa mara huenda nikawa namtafuta Asha kukidhi hamu..., kwahio upendo is a package ambayo kutamani ni ingredient ya hio package (subset).ukisema unatamani unamaanisha nini?