Swali la kizushi: Imekaaje hapa kwa CDF na RC

Swali la kizushi: Imekaaje hapa kwa CDF na RC

malela.nc

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2013
Posts
256
Reaction score
345
Habari wakuu. Hoja yangu ni nyepesi sana lakini inanitatiza kidogo. Tumeshazoea kuona CDF (Mkuu wa Majeshi) akipiga SALUTE kwa wateule wa Mh Rais. Hapa nazungumzia Mkuu wa Mkoa (RC)

SWALI:
Inakuaje pale Mkuu wa Majeshi anapoenda mikoa inayoongozwa na wanajeshi kama Kagera ulio chini ya Mh. Brig Gen M. Gaguti, nani anampigia SALUTE mwenzake kama wote watakuwa wamevalia mavazi ya kijeshi?
 
Mkuu hapo Gaguti akiwa kavaa 'kiraia' anapigiwa saluti na Mabeyo vizuri tu. Mkuu wa mkoa ni kama rais kwenye mkoa husika. Lakini ikitokea Gaguti akiwa kavaa 'kijeshi' hapo yeye ndo atampigia saluti Mabeyo, sababu ya mamlaka ya kijeshi
 
Mkuu malela.nc isije ikawa wewe ndo yule 'Malela' anaetafutwa miaka na miaka tangu alivyopoteaga Ruvu[emoji3] Au ni majina yamefanana tu mkuu?
 
Ni matatizo ya kuiendekeza siasa na kuchanganya mambo.
Amiri jeshi ni mmoja tu, apewe heshima anayostahili, hili la kuwapa heshima walioteuliwa na rais halina mantiki. Mkuu wa mkoa ni mkuu wa mkoa.
 
Ni..... Mkuu wa Mkoa Mh Brig Gen M. Gaguti. ✔

Sio..... Brig Gen M. Gaguti. Mh Mkuu wa Mkoa ❎
 
Back
Top Bottom