Swali la kizushi: Je, unaweza kumfundisha mwanao hesabu hadi darasa la ngapi?

Swali la kizushi: Je, unaweza kumfundisha mwanao hesabu hadi darasa la ngapi?

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,661
Reaction score
21,656
Tuseme Mtoto wako anapenda hesabu Ile balaa na anataka msaada wa baba/ mama.

Je, wewe kama mzazi unaweza kumpigia namba mpaka darasa la ngapi bila kudesa?
 
Siku hizi kuna youtube. Kama mzazi una elimu ya juu na unaamua kumfundisha mwanao inawezekana kabisa kuanzia la kwanza mpaka la saba.

Maana wewe unajifunza youtube kuhusu hiyo topic then unamfundisha mwanao
 
Kwa jinsi elimu ya sasa ilivyo nyoronyoro, mzazi aliyemaliza la saba mwaka 2000, anaweza kumfundisha mwanaye wa form 6 kwa sasa.
 
Integration & Differentiation....

Advanced BAM.
 
Tangu akiwa kindergarten. Ubongo wa mtoto unafanya vizuri sana kwa somo la hesabu akiwa mdogo. Wa kwangu nilianza kumfundisha hesabu akiwa 3 yrs (kindergarten), toka hapo alianza vizuri na kutoshuka kiasi cha walimu wake kumuita 'genius'.

Aliendelea hivyo mpaka kamaliza form six, sasa hivi yuko mwaka wa kwanza chuo kikuu. Kikubwa, mnunulie materials za hesabu, yeye mwenyewe atajenga mapenzi kwenye somo hilo kama 'hobby'.
 
Mi naona mzazi anatakiwa atoe miongozo na uwezeshaj mwingine,hayo ya utaalamu waachie wenyewe.Labda kama mzazi ni mwalimu
 
Tuseme Mtoto wako anapenda hesabu Ile balaa na anataka msaada wa baba/ mama.
Je wewe Kama mzazi unaweza kumpigia namba mpaka darasa la ngapi bila kudesa?
Mwisho wangu ni kujumlisha,kutoa,kuzidisha,kugawanya namba. Zikiingia herufi tu ndio mwisho wangu.
 
Back
Top Bottom