Swali la kizushi: Kwanini Diamond Platnumz na Wasafi festival wanakwepa mikoa ya Kaskazini..!!

Slowly

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
10,589
Reaction score
35,268
Tangu wasafi festival ianze last year sikuona mikoa ya kaskazin mwa Tanzania hususani Arusha na Kilimanjaro (Moshi) kama sehemu ya tour yao


Na sasa mwaka huu ratiba imetoka tena ya wasafi festival sijaona mikoa ya kaskazin


Kwa wale mlioko jikoni mtujuze kulikoni? Sababu ni nini?
 
Mbona kigoma ambapo ndio katokea diamond hawajawahi kufanya wasafi festival na kwenye ratiba ya mwaka huu haipo mbona huulizi? Kitu ambacho mtoa mada ujue mikoa ni mingi hawawezi wanafanya mikoa yote.
Kigoma huwez fananisha na moshi au arusha, ni halali kupiga chini kigoma kuliko Moshi na Arusha,
 
Hiyo ratiba ni ya Diamond na siyo ya Wasafi Festival,na Diamond alisema safari hii hatoperfom kwenye mikoa yote itakayofanyika Wasafi Festival

Subiri watoe ratiba ya mikoa inayofuata ndio uanze kulalamika!
Exactly ile schedule ya Diamond kama diamond sio wasaf festival...nauliza hivi FIESTA NDO IMESHAKUFA AU.KWELI BALAAA ZITOOO
 
Exactly ile schedule ya Diamond kama diamond sio wasaf festival...nauliza hivi FIESTA NDO IMESHAKUFA AU.KWELI BALAAA ZITOOO
Fiesta (tigo fiesta)haina nguvu kwa sasa kutokana imesha poteza wasanii wenye ushawishi mkubwa 2018 Vanessa na jux walikuja na yao (in love and money tour) halafuu wasafi festival ya diamond na timu take hivyo fiesta ikabaki na wasanii kama luludiva,whozu,weusi,jolie,jay melody etc ukizingatia walimtoa nandy
 
Hivi why walimtoa Nandy??
 
Kwa hiyo na diamond ni mbinafsi?

Alafu anaanzia muleba ? Bukoba vijijini huko

Labda kuna vibe Sana huko na sifa juu
 
Kigoma huwez fananisha na moshi au arusha, ni halali kupiga chini kigoma kuliko Moshi na Arusha,
Hamna vibe labda.

Kahama na muleba kuna nini pale.


Yaani wasafi festival inaanzia muleba Bukoba vijijini kabisa
 
Mi nimeona mikoa 4 tu hapo kwenye hiyo ratiba
Tanzania kuna mikoa zaidi ya 20 ila we unabaki kulia lia kaskazini
Ndio maana Nyie watu mnatuhumiwa wabinafsi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…