Swali la kufungia siku:Utafanyeje kuku wa jirani yako wakiingia uwani mwako?

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2016
Posts
4,580
Reaction score
7,943
Habari za jioni ndugu katika Mungu na katika baba wa taifa(Nyerere).
Wengi humu ndani wana nyumba ama wanatarajia kumiliki nyumba.
Je, kuku wa jirani yako wakiingia uani mwako au kwenye wigo wako utachukua hatua gani?
1.utachinja ule
2.utamtoza faini
3.Utawatimua na kumpa onyo
4.Utauza kimyakimya au utauza mbele ya halaiki ili umpe funzo.
5.Utawafanya utakalo na yeye utamwambia afanye atakalo pindi kuku wako watakapoingia uani kwake.

Naomba msaada wa jibu ambalo ujirani wenu utabaki imara.
 
Nimewahi siti ila hili swali ni la kipuuzi sana kuulizwa.
 
Mkuu daaah poleeee jaribu kuwa na broad analytical thinking utapata content ya mleta uz
Content si iko wazi unafikiri ikitokea hivyo kwa namna tunavyoishi huku uswahilini utafanyaje?na ndiyo maana nimesema swali la kipuuzi hili kuulizwa kwa great thinkers.
 
A house should not be built so close to another that a chicken from one can lay an egg in the neighbor's yard, nor so far away that a child cannot shout to the yard of his neighbor.

Mwl. Nyerere
 
Content si iko wazi unafikiri ikitokea hivyo kwa namna tunavyoishi huku uswahilini utafanyaje?na ndiyo maana nimesema swali la kipuuzi hili kuulizwa kwa great thinkers.
Kumbe ufahamu wako ni mdogo mno haukutoshi kuwa Great thinker, inaonyesha hukuwa msomaji wa novel au play mbalimbali.
Lugha ya picha ndiyo niliyoitumia hapa but wewe direct umekimbilia Uswazi kwenu.
 
Wanaweza leta magonjwa kwa kukuwangu kwaiyo nitawa...........kama wale
 
5.Utawafanya utakalo na yeye utamwambia afanye atakalo pindi kuku wako watakapoingia uani kwake.
Umenikumbusha story ya kweli aiseeee, miaka hio pale alipokulia Marehemu Shekilango, Mzazi mmoja mwanae alitofautiana na mtoto mwenzie wa jirani, dah, basi yule Mama akawa mkali balaa, akamuadhibu, akamlipizia kile alichotendwa na mwenzie, MUNGU sio John week ile ile wale watoto wakiwa wanacheza yule mtoto wa yule Mama aliyeumizwa kwa bahati mbaya si akamuumiza kwa kisu yule rafiki yake? Yule Mama wa jirani akachukua kisu akataka na yeye amkate yule mtoto kama alivyofanyiwa mwanae!! Ilikua aibu aiseeeeee, FUNZO, tafakai kabla ya kusema au kutenda because WORDS can Only be Forgiven not Forgotten.....
 
Hiyo ilikuwa hatari sana
 
Swali la kipuuzi kweli kweli la mleta uzi...
 
Swali la kipuuzi kweli kweli la mleta uzi...
Umeona jinsi wana fasihi tunavyoweza kumvua nguo mtu!!!
Ukilijibu swali hili kwa ufasaha basi utagundua kuwa tumempata kiongozi ambaye hata introduction to international Relation & Diplomacy hajui.
Lakini pia kwakuwa ulikuwa unakimbia novel na play darasani si ajabu hujui content ya uzi huu.
 
Kwakweli kama amenona atakuwq halali yangu...nampiga kimyakimya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…