Uhakika Bro
JF-Expert Member
- Mar 29, 2022
- 3,644
- 4,315
Zamani wakati ni mapyamapya kisukari na presha yalisemwa kuwa ni magonjwa ya matajiri. Je hilo limebadilika au kutokana na ukwasi wa watu binafsi kuongezeka. Na utajiri umekuwa kitu cha kawaida ndio maana sasa hivi tunasema ni magonjwa ya watu wote hata wa kawaida.
Tuliweke sawa hili jambo. Vijana wa 2000 pia tusikilizane kwa makini hapa;
Leo mimi nikimiliki pikipiki/boda sihesabiwi tena kuwa tajiri kama ilivyokuwa miaka ya zamani. Miaka hiyo kulikuwa hakunaga gari kabisa mtaani na pikipiki unazoziona labda wale mabwanashamba na wenye helahela kweli. Leo mmiliki wa boda anahesabiwa kama bado anaungaunga maisha sio tajiri.
Lakini ambacho hakijabadilika absolutely ni kwamba ana mali na anailinda hata kama relatively hatujamuweka kwa matajiri. Tukitumia kipimo absolute mimi nasema huyu ni tajiri na akisumbuliwa na sukari au presha anakuwa anapambana na ugonjwa watu kama yeye haswaa - Matajiri
Kimsingi kiasili mnyama aliye katika kulinda mali zake/wanae au kujilinda mwenyewe huwa anatahayari(flight or fight)
Mnyama aliyetahayari husukuma damu kwa presha kubwa ili iifikie misuli kupeleka chakula na damu. Mnyama huyu hupandisha kiwango cha sukari kwenye damu maana ndiyo chanzo cha nishati cha ubongo na misuli pia.
Jambo hili likitokea kwa muda mfupi ni afya tu, atapona atakapopumzika (rest mode). Ubaya ni pale atakapoendelea kukaa na hali hiyo ya kujihami kwa muda mrefu ndiyo tunasema ana kisukari au presha.
Swali la kujiuliza; Je nina uhusiano gani kiulinzi na mali zote ninazomiliki. Nimejihami na sijauamini ulinzi? Au nina uhakika na ulinzi uliopo na nimerelaax? Au kwanza similiki chochote kwa hiyo sijihami wala silindi chochooote?
Hizo mali tunazolinda zipo katika hali zote ikiwamo watu, mali na itikadi mfano;
Mfano 1. Je mke niliyenaye ninamuamini wala sihangaiki kumlinda? Au nipo naye hatihati anaweza kupotea kwa hiyo kila mara nimejizatiti vilivyo? Je watoto wana akili au hadi nizunguke na helikopta kuwatizama kila mara?
Mfano2. Biashara, kazi, uwekezaji nilionao vp? Mkulima anaweza kuwa makundi mawili, (a) anayeamini kuwa shamba lake lipo salama na mvua itanyesha atalima- halindi
(b) anayehisi mvua hazieleweki na hata mipaka ya mashamba majirani mda wowote wanasogeza - in short ako na vita kuu.
Mfano3. Hata vitu binafsi unavyomiliki kama afya, je unajiaminisha kuwa una afya kutokana na lifestyle, matunda, mazoez mboga? Au umejiaminisha kwamba huna afya ila unapambania kuipata kwa lifestyle etc?
Nnazungumzia ile attitude tu wala sio tukio lenyewe. Mfano umepelekwa jeshini kwa mujibu wa sheria. Ni jukumu lako kuchukulia yale kama mazoezi ya kukujenga tu (relaax), au kuchukulia kuwa ni mateso ya kukuumiza tu (vita).
Hata dini tulizonazo je umerelaax kwamba nguvu zisizoonekana zinakupigania au upo vitani na nguvu zisizoonekana zinashindana na maisha yako? Au mali zako za kiroho zimetulia haziondoki? Au unawaza kuna kinyamkera kitazichota usipozilinda?
Thread imekuwa ndefu ngoja tuhitimishe kwa nadharia:
Presha na sukari hubakia juu kwa mtu anayehitaji kulinda 'mali' zake muhimu zisipotee. Ndio maana ni ngumu kukuta matatizo haya kwa mwenye akili ya kutohitaji kun'ga'ngana na chochote (egoless) kama monk wa kiBudha, au rastamani wa Buza😎. Maskini in material sense.
Welcome....