Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele ‘Maslahi ya Taifa’?

hakuna uovu unaojenga taifa, hakuna uongo mzuri kaka, kama hakg ndio huinua taifa kwenye haki hakuna uongo nikweli
Mkuu nyembela , bandiko hili halizungumzii uongo mzuri, linazungumzia ukweli mchungu ambao haupaswi kusemwa!.
Hapa tofautisha Chama, serikali na hulka binafsi za viongozi. Kwa CCM ni chama cha haki, kusema ukweli daima, fitna kwake mwiko.
Naunga mkono hoja kuwa kila uongo lazima usemwe, ila sio lazima kila ukweli usemwe!.
P
 
Mkisikia civility, ndio hii, kiukweli Freeman Mbowe ni gentleman. Mtu kuzaliwa familia bora, malezi, makuzi ya kistaarabu, huwezi kuwa ropo ropo. Linganisha angekuwa yule msomi wetu...

Compare and Contrast Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?
P
 
Kwenye hili la kupayuka na kuropoka kila unalolisikia,kaka zake tupo,tutamsaidia mdogo wetu ,sio lazima kusema kila unachosikia hata kama ni kweli!。
P
 
Kwenye hili la kupayuka na kuropoka kila unalolisikia,kaka zake tupo,tutamsaidia mdogo wetu ,sio lazima kusema kila unachosikia hata kama ni kweli!。
P
Heshima yako mkuu ktk hili saga linaloendelea nilikuwa nasubiri sana mchango wako. Natumaini utakuja na bandiko murua.
 
Kwenye hili la kupayuka na kuropoka kila unalolisikia,kaka zake tupo,tutamsaidia mdogo wetu ,sio lazima kusema kila unachosikia hata kama ni kweli!。
P
Kwa sasa huna moral probity ya kueleza hayo unayoeleza kilichobaki ni wewe kutoa maoni katika upande wako kama private citizen.

Hayo unayoyasema 2016 ndio ningeweza kukusikiliza ila kwa sasa is a big NO.
 
Kama unaandika kwa kuelimisha Jamii kusema ukweli ni jambo jema, hata hivyo uamuzi wowote utakao ufanya maishani mwako utawajibika nao, (any decision you make in life you will be responsible for it), vile vile viongozi wa kitaifa inatakiwa watunze kali zau, (public figures have to keep their words)
 
Kwa sasa huna moral probity ya kueleza hayo unayoeleza kilichobaki ni wewe kutoa maoni katika upande wako kama private citizen.

Hayo unayoyasema 2016 ndio ningeweza kukusikiliza ila kwa sasa is a big NO.
Mimi ni mwalimu muelimishaji umma,baadhi ya mabandiko yangu ni mabandiko shamba darasa, bandiko hili ni darasa tosha kwa wanaopenda kujifunza,ila pia ni mwiba kwa wahafidhina。
P
 
Mimi ni mwalimu muelimishaji umma,baadhi ya mabandiko yangu ni mabandiko shamba darasa, bandiko hili ni darasa tosha kwa wanaopenda kujifunza,ila pia ni mwiba kwa wahafidhina。
P
Pole sana!

Huo mwiba wako utaishia kutoboa puto.

Labda wasiokujua unafanya kazi kwa niaba ya nani.

Heshima yako uliyoijenga kwa miaka mingi umeivunja mwenyewe, nenda kwenye kioo ujiangalie utamuona adui yako.
 
Askari huambiwa sio kila kitu cha kusema/kujibu public.
Tuishi humu
 
Baada ya EK kutoa kitabu chenye maukweli fulani makubwa, nimelikumbuka bandiko hili, sio kila ukweli lazima usemwe!, ukweli mwingine ni ukweli wa hatari, unaumiza, unaamsha machungu, na kutonesha makovu, haswa ukweli huo unapotoa picha ya mtu ambaye siku zote ulimuona ni malaika halafu leo uambiwe ni shetani!。

Kama mhusika ameisha tangulia mbele ya haki hivyo hawezi kujitetea,nashauri ukweli unao mbagaza marehemu kwa ubaya,usiwekwe hadharani,huku ni sawa na the consecretion of the dead!, aachwe apumzike!。
P
 
Yaani kuwa rafiki na Eric kabendera ndo inatosha kabsa kutuaminisha kuwa anasema ukweli?!!
Hizi sifa unazopewa hapa jf zinakufanya ujione uko sahihi sana na kila unachofikiri Kiko sawa!!!?

Eric kasema kaambiwa hao waliomwambia unasema hawapaswi kutajwa!! Je kwann iwe ni kweli??!

Ulisema umetoka familia ya tiss, basi unaamini unajua sana mambo ya tiss kwakuwa familia yako imetoka huko na una mambo ya ndani??!

Unatuthibitishia kuwa Ben alipigwa risasi kichwani na magu mwenyewe???

Unatuthibitishia kuwa magu alitaka kumbaka samia??!

Unatuthibitishia kuwa magu alikuwa kichaa na ccm wakampitisha kugombea urais?!!!

Huu ukweli wa kabendera kwann unataka tuuanini au kwakuwa wapo wanaohisi ulimuuza jamaa kipindi kile 2017??!

Unatuambia kama hatuna ushahidi basi hatuna moral authority ya kupinga, ila unataka tukubali shutuma zisizo na ushahidi??!! Ati kwa kuwa Eric ni investigative journalist!!!

Akiitwa investigative journalist basi inatosha kuwa msahafu tuuamini??!!
Sympathy zako kwa Eric zisikufanye ukajiokotea dhambi za burebure ati kisa umempigia simu akakwambia ni kweli alichosema!!

Karma is really as you say, it'll beat someone, soon!!!
 
Yaani kuwa rafiki na Eric kabendera ndo inatosha kabsa kutuaminisha kuwa anasema ukweli?!!
Narudia kwa msisitizo,EK is one of “the best of the best that we have” kwenye waandishi wa IJ,kazi ya uandishi is telling nothing but the truth,amefanya IJ yake kajiridhisha kaandika,sisi tunao muaminia tunajua kasema kweli,wahusika wanajua amesema kweli,japo maelezo mengine hayajanyooka。
Hizi sifa unazopewa hapa jf zinakufanya ujione uko sahihi sana na kila unachofikiri Kiko sawa!!!?
kiukweli sijawahigi kulewa sifa,sijawahi kujiona niko sahihi sana,na sio kweli kuwa kila ninachofikiria kiko sawa!。
Eric kasema kaambiwa hao waliomwambia unasema hawapaswi kutajwa!! Je kwann iwe ni kweli??!
Kazi ya uandishi is getting info,kutoka sehemu mbalimbali kwa watu na sources mbalimbali,some of the sources ni trusted sources, hivyo ukipata info from trusted sources,you dont have to doubt utajua ni kweli tupu,japo ni kweli sometimes a trusted source inaweza kukupa fake info,some ni hoax,some ni dupe。Kila kazi ina rules zake of the game,miongoni mwa the rules of the game za journalism ni kipengele cha ”the confidentiality of the source”,mwandishi una wajibu wa kumlinda source wako, kwenye kashfa ya watergate,the source alikuwa ni mtu wa ikulu,kwa jina la “deepthroat” mhariri wa gazeti la The Washington Post,alilinda the identity ya reporter wake, anayekuwa fed info na deepthroat,alikubali kwenda jela kulinda the identity ya source wao。 hivyo EK akishitakiwa,for sedition atakuwa tayari kwenda jela kuliko kumtaja source wake wa ikulu。
Ulisema umetoka familia ya tiss, basi unaamini unajua sana mambo ya tiss kwakuwa familia yako imetoka huko na una mambo ya ndani??!
ni kweli mimi ni born and breed from Tiss parents,baba na mama,sijasema najua sana mambo ya ndani ya Tiss, kwanza kuja kujua baba ni Tiss, nilisoma gazetini gazeti la Mzalendo,nikiwa darasa la 5!,dingi ana kesi ya mauaji Mwanza!。 Mama nimekuja kujua nikiwa form 5,Arusha,mama akahamishiwa Arusha,nilipoonyeshwa kazini kwa mama,watu wanajua hilo jengo!。Sikuwahi kujadilichochote cha Tiss na mzazi wangu yeyote!。 Bali nilisema humu ukizaliwa na wazazi wako wote wawili ni Tiss,unakuwa umezaliwa na natural inteligence ya ki tiss tiss,na damu kwenye veins zako inakuwa na vi elements vya ki tiss tiss, unakuwa na security conscious ya ki tisitisi, hivyo ukiyaona haya majinga ya sasa wanafanya ujinga ujinga,unajotolea kuwaamsha kwa kuwafunda TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!

Ile August 2014, ni mimi ndie nilitangaza humu ujio wa JPM kuja kuwa rais wa Tanzania Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli nikasema nimepenyezewa hii na mtu from deep inside。nikasema nimeelezwa sababu why ni ni Magufuli,nikasema nitazitaja hizo sababu。
Kwenye bandiko hilo pia niliweka reservations zangu, na zikaja kutokea zote, moja baada ya nyingine!。
Na kwa vile mimi ni mzalendo wa kweli wa nchi yangu,nikawa kila nikikutana na kitisho chochote cha kiusalama,nakileta humu kwavile najua kuna ma tiss wakutosha tuu humu wametamalaki!。mifano ni hii
its very unfortunately yale majitu majinga ajabu,yalishindwa kum protect mtu wetu!, akatwaliwa!
Ili kumprotect huyu aliyepo,huwezi kuyategemea majinga haya,nimeamua kumsaidia kwa kumweleza yeye mwenyewe humu humu ambapo anapita mwenyewe kwa kitu kama sauti HII
Unatuthibitishia kuwa Ben alipigwa risasi kichwani na magu mwenyewe???
Mimi nithibitishe kama nani?。 Ninacho thibitisha humu ni namjua EK,ni mwandishi wa IJ za ukweli,EK, kaandika ukweli wa alichoambiwa, wenye ukweli tofauti walete to compare notes!
Unatuthibitishia kuwa magu alitaka kumbaka samia??!
Nithibitishe hili mimi nani, hukumsomaga yule kichaa Mange alipoliweka,unashangaa leo EK kalisema!。
Unatuthibitishia kuwa magu alikuwa kichaa na ccm wakampitisha kugombea urais?!!!
Nenda kayasome mabandiko yangu haya mawili huku umetulia Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli na Kuwa kichaa sio mpaka kuokota makopo! Je, Tanzania tuna vichaa wengi kuliko tunavyojidhania? kisha jibu utalipata mwenyewe
Huu ukweli wa Kabendera kwanini unataka tuuamini au kwakuwa wapo wanaohisi ulimuuza jamaa kipindi kile 2017??!
Sijasema nataka tuuamini,kuamini ni individual,ninachosema namjua EK,ni mkweli, mimi namuamini, kila mtu ana uhuru wa kuamini anachoamini,hili la mimi kumuuza EK ni kweli nilihisiwa,alipofiwa na mama, kwanza nilimuombea kwa JPM Personal Plea Kwa Rais Magufuli: Kama ameweza kuwasamehe wabakaji, wauaji, mafisadi, wahujumu, anaweza pia kumsamehe Eric Kabendera, amzike mama yake
Mimi ni miongoni mwa waandishi tuliomzika mama yake EK, kisha nikajibu tuhuma Pascal Mayalla ndiye aliyemchongea Erick Kabendera kwa dola
Nikiwa UK, nikamtafuta,akanijulisha jinsi alivyokuwa akipelekewa print out za jf jinsi ninavyomchomea!。 Thanks God he is an intelligent man,angekuwa mjinga mjinga angeamini huo ujinga!
Unatuambia kama hatuna ushahidi basi hatuna moral authority ya kupinga, ila unataka tukubali shutuma zisizo na ushahidi??!!
hapana nimesema EK ni mkweli ameambiwa na trusted sources ndio maana kaandika,kama kitu hukijui huwezi kumbishia anayekijua,unless ulete unachoju wewe。
Ati kwa kuwa Eric ni investigative journalist!!!
Akiitwa investigative journalist basi inatosha kuwa msahafu tuuamini??!!
Sijasema ni msahafu,kama hata Samia anadanganywa,itakuwa EK?。Nimesema na nitasema tena na tena na tena,EK ni one of the best we have interms of IJ
Sympathy zako kwa Eric zisikufanye ukajiokotea dhambi za burebure ati kisa umempigia simu akakwambia ni kweli alichosema!!
Huwezi kuchuma dhambi kwa imani bali matendo, mfano hata kama huamini Mungu kuwa mpagani sio dhambi,dhambi ni kuamini miungu wengine!。huwezi kuchuma dhambi kwa kuamini ukweli wa EK, na hata kwenye imani zetu za dini Angalizo: Kuna Wengi Wanamwabudu Shetani Wakidhani ni Mungu!. Jee Wewe Unajijua?, Jitambue!.
Karma is really as you say, it'll beat someone, soon!!!
hili tunakubaliana na wewe。

p
 
Mkuu paskal, nmesoma nimeelewa sehemu ya hoja zako!!

Nakubaliana nawe, ujinga wa wale watu!! Wengi ni watoto wa....

Ni kweli walishindwa kumlinda, nakubaliana nawe katika Hilo!,

Nakubali pia kuwa umejitahidi sana kumlinda blaza wako, japo kaunafiki ulikuwa nako ila, naheshimu Hilo!!

Ila hii ya kusema "vyanzo kutoka serikalini na upinzani viliniambia" mtu yoyote aweza sema!!! Huo sio ushahidi kamili wa kuaminika, ni kwa vile mtajwa mkuu hayupo basi ni rahisi kusema lolote lile!!

Kusema kwamba, ni one of the best IJ sikatai kwakuwa ni mtazamo wako!!! Kwa wengine ni just another...... Katika Ile Ile cycle Fulani mahali Fulani huko!!!

Kusema kwamba hata akishtakiwa kuwa awataje waliompa taarifa(za uongo wa kujitungia), atakubali kwenda jela, hii ndo itathibitisha kuwa ni muongo wa kutupa, sio kila IJ akija na hearsay zake tuamini maana ana kile kitu kinaitwa "confidentiality of the source" zingine ni chill source tuu!!

Walianza akina meena, watakuja wengi, ila Ganda lazma litaisha utamu muda si mrefu na litatupwa tutaanza upya!!

Japo karma sometimes huchelewa, na pengine hutokea hata pasipo mtu kujua ila lazma itakula, na ishaanza tayari, tujipe muda kidogo harufu itatoka kutokea huko mpaka huku!
 
Mkuu paskal, nmesoma nimeelewa sehemu ya hoja zako!!
Asante
Nakubaliana nawe, ujinga wa wale watu!! Wengi ni watoto wa....!!
Ni kweli, zamani walikuwa wa recruit watoto wao kwa imani watakuwa wazuri kama wazazi wao, but its very unfortunately, wazazi wazuri wanazaa mitoto mijinga ajabu!.
Japo karma sometimes huchelewa, na pengine hutokea hata pasipo mtu kujua ila lazma itakula, na ishaanza tayari, tujipe muda kidogo harufu itatoka kutokea huko mpaka huku!
Hili la karma, nakubaliana na wewe, uzuri wa karma, ukiishalipa deni la karma, deni linafutwa, hivyo JPM ameisha lipa deni lote la karma yake saa hizi yuko peponi!.

EK naye, kama amedanganywa na yeye akaandika, huko ni kumsingizia marehemu!, karma yake inamsubiria.

Ila hata kama ni kweli, hakupaswa kuandika kila ukweli, kuna ukweli mwingine ni ukweli wa kuaibisha kama ule ule ukweli wa kushusha kisago kwa wife au ile ya kuibuka mahali na pyajama!, hizo ni personal private issues ambazo ziko covered and protected by the right to private. He just said too much!.
Viongozi wetu pia they are human beings, na wanaruhusiwa kukosea, na sisi Wasukuma, wanawake kwetu is not a very big deal!, hivyo mama kuchezea kichapo ni kawaida sana, hata wangu tukiwa bongo, amechezea, tulipohamia US, akanichenjia na kuambiwa "thubutu“ , au ukisikia njaa, sio lazima kuomba chakula, unajichukulia tuu na kujilia, anataka hataki!, kule US lazima uombe na ukubaliwe ndipo upakuliwe!. Hivyo vitu vingine ni tuu personal!, hata ningekuwa mimi, mfano unaweza kukuta jamaa alikuwa na udhaifu kama wangu Ikitokea kuna Kiongozi ana Macho mazuri, na umeyapenda, je, kuna ubaya kumsifia macho yake? Ni ukosefu wa heshima na adabu? halafu inatokea wewe ndio baba la baba, unaweza kughafilika!, mambo ya trivia hakupaswa kuyaandika!.

P
 
P,

Kama umesha angalia vizuri watu wa 60 kama Mbowe na wa chini ya 60 kuna tofauti na jinsi ya kuchukulia mambo. Urembaji kwa uandishi wako na approach kama za Mbowe zinaendana sana.

Kitendo cha serikali na chama kuhusisha
Usalama na Polisi ni game changer sasa tutaona kuanzia waandishi mpaka wanasiasa wengi wanakuwa zaidi mapiganaji. Msishangae kuona kitabu cha Magu kimetoka na mapambano ndani ya Chadema yanaenda kwenye misimamo mikali kama nilivyo tabiri kuna shift Vijana wengi sasa wataanza kufikiria nchi na mifumo na sio watu

Kwa ufupi watu kama wewe na Mbowe ambao wanatumia busara sana hiyo approach itakuwa tested mwaka huu . Upinzani sasa wanaingia majembe kweli kweli
 
Nahisi kama sijaelewa au ndio uzee
P
 
Sio Lazima kusema kila ukweli

Busara is to chose and filter what is for public consumption and what is not
 
Kwa ufupi uandishi wako una fanana na Mbowe. Lakini nasema hiyo approach inabadilishwa sasa na wakina Lissu, Mpina, Heche, Lema, Msukuma …. ambao hawana uvumilivu
Kweli enzi za kiti moto nilikuwa moto nina nyoosha, baada ya kuhudumu ubalozini, nimekuwa a diplomat, ninaandika very diplomatic.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…