Swali la Mwandishi Wa Habari Kwa Msemaji Wa Simba

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Umewezaje Kwa muda mfupi kufanya mambo makubwa ndani ya Simba?

Jibu ni jepesi tu haya ninayofanya niliyasoma darasani kwenye Topic ya PR Campaign

Kama PR hujapita darasani huwezi kufanya vitu vidogo kama hivi baadala yake utahangaika na maisha binafsi ya watu

Ni rahisi kumuona PR ambae hajapita darasani anakagua SAUTI za Watu kisha anasema fulani anabana pua ni kwa sababu hana Campaign yoyote wala Strategy ya kufanya kwenye kazi yake

Ni rahisi mno kumuona PR ambae hajapita darasani anakagua SUTI za watu na kugundua aina ya kitambaa kwa sababu hana mpango kazi wa kufanya ndiyo maana anahangaika na mavazi ya watu

Ni rahisi sana kumuona PR ambae hajapita darasani anazungumzia sehemu wanazoishi watu kama Kijiwe Samli kwa sababu hajui kaajiriwa afanye kazi gani.

PR sio kipaji cha kuzungumza ni taaluma ambayo watu wanakaa darasani miaka mitatu kutafuta ujuzi.

Kijana mwenzangu mwenye ndoto ya kuwa PR usifanye mazoezi ya kuongea kwa nguvu nenda darasani tu.

Sidhani kama kweli alisoma vizuri PR yake maana nae amejibu kimajungu tu.
 
Wakati anahojiwa hakusema maneno yote hayo,ila hayo maneno mengine mengi kayaongeza ktk Instagram wakati anaelezea jinsi alivyoulizwa hilo swali..alikuwa anafafanua vzr kile alichojibu kwa mwandishi kupitia page yake ya Insta.
 
Ukiona Haji alichokoment kwenye post ya Makonda juzi, Hata alivyokuwa anawananga waandishi wa Habari, pia povu alilokuwa anawatolea Nugaz na Jerry Muro siku za nyuma utagundua huyu jamaa Kaongea ukweli.
 
Umewezaje Kwa muda mfupi kufanya mambo makubwa ndani ya Simba?

Jibu ni jepesi tu haya ninayofanya niliyasoma darasani kwenye Topic ya PR Campaign...
Hahhahaah dah mbona hata yeye tena kajibu kwa majungu sasa hiyo PR iko wapi sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…