Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Huu mchakato nilishadokeza kuwa ni mchakato mbovu; hapa najaribu kuonesha jambo jingine. Mawaziri Wote na Manaibu Wao ni Wabunge wa Bunge la Katiba. Hapa nazungumzia Mawaziri wa Serikali ya Muungano na wale wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar! Tofauti na Bunge la Kawaida, hawa hawaingii kama wasemaji wa serikali na hawatosimama kuulizwa maswali na wabunge na watoe majibu. Kwenye Bunge hili wanaingia kama wajumbe wengine tu na wakiwa na sauti kama wabunge wengine.
a. Pamoja na Mishahara yao ya Mawaziri na Ubunge (sijui kama wanalipwa yote) watalipwa pia posho za Bunge hili (kama Rais atakuwa ameridhia). Sawa?
b. Kwa sababu Bunge hili litakuwa na vikao karibu vya miezi mitatu (sijui litakuwa linakutana kwa mfumo upi tusubiri) lakini vyovyote ilivyo Mawaziri na Manaibu Waziri itabidi na wao wajitahidi kuhudhuria vikao hivi kwani ukijumlisha utaona kuwa peke yao ni karibu 1/6 ya bunge la Katiba!
c. Vikao vya Baraza la Mawaziri itabidi vipangwe kuzingatia Bunge la Katiba au vikao vya Bunge la Katiba itabidi viaccommodate vikao vya Baraza la Mawaziri (ambavyo kwa kawaida hufanyika kila wiki). Na kwa vile Bunge linafanyika Dodoma, Mawaziri nao watakuwa wanakutana vipi na Marais wao; kumbuka kuwa hata Waziri Mkuu ni mjumbe wa Bunge la Katiba!
Hapa inabidi kujiuliza mfumo wa utendaji kazi wa serikali zetu utakukuwa vipi wakati wa Bunge hili la Katiba? Au kutakuwa na 'excuses' nyingi za hawa kutohudhuria lakini watakuja siku ya kupiga kura?
Mweh "magenius wetu" hawa...