Heshima kwa babu;
Wadau hebu jaribuni hii kitu "The Construction of Social Reality/ The Social Constructionism" (Luckman & Berger; 1966) ina insights flan ambazo zaweza toa one among the perspectives
majina ni kirahisisho cha kurejea tu mtu fulani,mimi kwa watoto wangu ni mama tough wanalijua jina langu vizuri tu!marafiki zangu napenda waniite jina langu la kwanza lakini mume wangu sipendi aniite jina langu,akitumie pet name yangu ndo naona ni nzuri zaid.ndo mana sina hakika sana na kusema ni sahihi mtu yeyote kukuita jina lako,lakini hii sasa ni tofauti na wale wanaotumia vyeo au elimu zao kwa mfano kujitambulisha ,tena inakera zaidi inapokuwa ni katika mazungumzo.things like,my name is Prof Kibakuli Kimejaa,its too rude!and immature to be frank.
Hata Google waeza pata Book Summary Babu
Inakera sana ndugu yangu snowhite,
Napo hajawatajia alivyomaliza PhD yake ya Uchumi au Uhadisi huko Missouri 1971 eti kabla wengi wenu hamjazaliwa!!
Waafrika wengi wamekuwa malimbukeni wa haya mambo. Nashindwa kuelewa kwa nini wanacopy na kupaste kila kitu kutoka kwa walimu wao isipokuwa adamu ya kujitambulisha mbele za watu!!!
Babu DC!!
Ngonja nijaribu kamanda wangu Ole wa Saidimu!!
Uzee huu unatufanya tuendelee kutumia baiskeli wakati kuna bajaj!!
Hujawahi kukutana na mtu kabeba mzigo wa kuni kichwani huku kapanda kwenye Fuso??
Babu DC!!
Ha ha ha babu huachi vituko bana......nakumbuka kuna siku nimemuona mtu kapanda kwenye basi na kuku halafu kampakata tuuuuli kuku wake kamtia kwenye rambo kichwando kipo nje......natamani nimwambie mama kuku si umuweke chini........lakini kila nikimtazama uson sion button ya welcome note...............
Jamani msitucheke bwana,
Haya mambo ni mageni kwetu kama ambavyo hawa vijana wa dot com watakuja kuwaogopa jongoo na viwavi kama vile ni chui au fisi wakati sie enzi zetu tulikuwa tunakimbizana na simba na nyati maporini!!
Babu DC!!
Ha ha ha babu huachi vituko bana......nakumbuka kuna siku nimemuona mtu kapanda kwenye basi na kuku halafu kampakata tuuuuli kuku wake kamtia kwenye rambo kichwando kipo nje......natamani nimwambie mama kuku si umuweke chini........lakini kila nikimtazama uson sion button ya welcome note...............
Haya ndo yalisababisha eti wabunge wanajiita mheshimiwa,akiitwa kwa jina lake bila hako ka mheshimiwa anajaa gesi!!
Kakunja sura kama anakamuliwa jipu!!