Swali : Nimeulizwa

Kimbweka

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2009
Posts
8,597
Reaction score
1,690
Nimeulizwa swali na mdada mmoja inaelekea kuna shida amempata (sikupenda kudadisi zaidi) na sijampa jibu kamili.
Mara nyingi na inaendelea kutokea hadi leo kwamba kwenye mahusiano kukawa na ugomvi na matokeo ya ugomvi inakuwa ama kuumizana/kuumizwa (physically) au kuharibu vitu ama kuharibiwa hasa kwa wale walio katika ndoa (kuvunjwa vioo vya gari, kupasua tv n.k). Na inapotokea hivi, ambapo kwa wahusika, anayeona kaumizwa / kaharibiwa vitu (pengine hata kuchomewa nguo) kaenda shitaki kwenye vyombo vya usalama wa raia kesi zake huwa hazifikishwi mahakamani na huambiwa wakamalizane wenyewe wao kwa wao tofauti zao.

SWALI:

  • Je hii ni sahihi?, maana hukumu hutolewa kwa mujibu wa sheria na mahakama
  • Kama si sahihi ni jambo gani linapaswa kufanywa/kufuatwa na mshitaki ili haki yake itendeke?
 
Mwaka 2004 mpenzi wangu alivunja vitu vingi nyumbani kwangu na kuligonga gari langu kwa kutumia lake,nikamshitaki polisi wakaenda kumkamata alipoletwa polisi wakakataa kufungua jalada wakadai tumalize wenyewe eti ni ugomvi wa wapenzi.Alidai eti ana mimba inamsumbua na kufanya vitu vya ajabu kumbe ilikuwa janja yake kuua kesi,mambo ya mapenzi uyasikie tu yana upande mbaya.
 
Jamani tatizo mahakama zina misululu ya kesi za msingi na hazijasikilizwa. Shida ya kesi za wapenzi unaandika leo kesho wanakuja wameshikana viuno wanataka kuifuta. Na cku zote serikali inapenda kumaliza kesi za kawaida kwa njia mbadala.
 
Makosa uliyotaja yapo katika kundi la makosa ya jinai. Mtu yeyote anayevunja sheria, sheria inataka afunguliwe mashitaka na kufikishwa mahakamani. Kufikisha kosa kituo cha Polisi ni haki ya kila mtu na Jeshi la Polisi halina nguvu kisheria kukataa kufikisha shitaka mahakamani. Mara kadhaa baadhi ya maofisa Polisi wamekuwa wakifanya kazi ya mahakama kwa kujaribu kutoa uamuzi hata kufanya mazingira ya kuwachiia watuhumia pamoja na kuwepo vithibitisho/vielelezo vyote dhidi ya mtuhumuiwa, hali hii ni baadhi ya mambo yanayochangia uhalifu uendelee kuota sugu. aidha maofisa wa Polisi wanaofanya vitendo hivi wengi na ni wale ambao hawafahamu hatari na hatua ambazo wanaweza kuchukuliwa kama mhusika ataweza kuwasilisha malalamiko yao kwenye ngazi za juu za jeshi la Polisi au hata mahakama. Kwa mtu yeyote ambaye atafikisha shitaka Polisi na kuona kuwa Polisi ana njama za kutaka kutoa uamuzi au usuluhishi kinyume na utaratibu wa kisheria, wasiishie kituoni hapo ila wawaripoti mara moja kwa viongozi wao wa juu kama mkuu wa kituo au OCD au kufikisha malalamiko yao makao makuu nya jeshi la Polisi ambapo kuna kitengo maalumu cha kusikiliza malalamiko dhidi ya Polisi wanaokwenda kinyume na taratibu zao za kazi. Aidha wakati mwingine Polisi huamua kujaribu kusuluhisha kesi za wanandoa katika hatua za awali kutokana na wanandoa wengi kutaka muafaka mara kesi zinapokuwa zikiendelea mahakamani, kitu kinachotoa usumbufu mkubwa kwa jeshi la Polisi pamoja na mahakama. Hivyo magomvi yanapozuka kati ya wanandoa, kabla ya kuyapeleka kituo cha Polisi kuwe na dhamira endelevu pamoja na kuwa tayari kwa hukumu ambayo inaweza kutolewa na mahakama kama itabaini kosa.
 
Lakini hii si ni domestic violence je kuna anayejua sheria
zetu zinasemaje kuhusu haya mambo?
 
Lakini hii si ni domestic violence je kuna anayejua sheria
zetu zinasemaje kuhusu haya mambo?

Sizijui sheria vizuri ila kesi za mapenzi, ndugu, mke na mume ukipeleka polisi ni sawasawa na kupoteza muda watasikiliza halafu baadae wanawaambia mkamalizane wenyewe. Mtoa mada mshauri tu huyo dada aachane nayo asijaribu kupoteza muda kabisa polisi hawazifuatiliagi hizo kesi hata uhonge kiasi gani ni kupoteza muda na pesa zako tu
 
Jamani tatizo mahakama zina misululu ya kesi za msingi na hazijasikilizwa. Shida ya kesi za wapenzi unaandika leo kesho wanakuja wameshikana viuno wanataka kuifuta. Na cku zote serikali inapenda kumaliza kesi za kawaida kwa njia mbadala.

Ina maana hizi siyo kesi za msingi?
Mwizi aliyeiba kuku au ng'ombe ndo unaiita kesi ya msingi?
Think the other way round!!!
 
kwenda polisi hapa Tanzania wakati mwingine ni kupoteza muda na hela.....

kuna means nyingine tu za kusuluhisha na mtuhumiwa kulipa alivyoharibu.......!!!
 
kwenda polisi hapa Tanzania wakati mwingine ni kupoteza muda na hela.....

kuna means nyingine tu za kusuluhisha na mtuhumiwa kulipa alivyoharibu.......!!!
Tutajie ili tusiwe tunapoteza muda.
Maana ukifika hapo wanasikilizia kama kuna mwanya wa kukutoa chai.
 
wewe ukitaka haki yako sema humjui huyo mwanamke....

amekuvamia na wala hujui katumwa na nani....

utapata haki yako.........
 
Kuna watu vimeo humu,tv nini bwana mpaka ukamshtaki mpenzi wako....
 
Peleka hii thread jukwaa la sheria. Kuna wanasheria kule huku hawatii mguu.
Wengine humu tunajua sheria zimewekwa ili zivunjwe ili polisi na usalama wapate ajira.
 
wewe ukitaka haki yako sema humjui huyo mwanamke....

amekuvamia na wala hujui katumwa na nani....

utapata haki yako.........
Nimecheka hadi basi una roho mbaya lol!

Kuna watu vimeo humu,tv nini bwana mpaka ukamshtaki mpenzi wako....
Hayakukuta ndio maana wangu alivunja kila kitu,gonga gari na nilimkuta anataka kuchoma nyumba ya kupanga yote eti sipo hewani.

Peleka hii thread jukwaa la sheria. Kuna wanasheria kule huku hawatii mguu.
Wengine humu tunajua sheria zimewekwa ili zivunjwe ili polisi na usalama wapate ajira.
Dah! Hus wangu niwewe kweli ?
 
Kwa mke au mme ni ngumu, jaribu kulipeleka kwa ndugu na sio polisi haraka hivyo, unaweza tengwa na ndugu unless upo tayari kwa hiyo hali ya kutengwa

Kwa wapenzi ambao haujafikia hata uchumba peleka polisi tu, ila sasa wapelelezi wakigundua ni wapenzi huwa hawahangaiki na kesi za hivyo, sijui ufiche vipi huo uhusiano
 
Tulikosana na wife kaenda polisi mara kadhaa wanamtupa nje,mimi bado nampenda.akatumia shinikizo la wakubwa kwa sababu aunt yake anafanya ofc ya waziri mkubwa jarida likafunguliwa polisi,wakanipigia cm niende,eti ninashitaka la kujibu,sikwenda,nasubiri waje kunikamata.hapo ndo mwisho wa ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…