Je kuna mtu ambaye anatumia mtandao mwingine zaidi ya Voda ambaye amepata ile msg ya kumkashifu Slaa inayotoka kwenye namba ya kughushi, yenye code fake ya Finland, moja kwa moja?
Imeonekana kuwa wengi wanaopata msg hii directly kutoka katika hii namba ya kugushi ni wanaotumia mtandao wa voda, kisha inasambaa katika mitandao mingine ikitokea namba hizo za voda...
NB: Ile namba ni fake na imetengenezwa hapa hapa Tz. kwani namba za Finland baada ya code number (+358), zinafuata Trakimu tisa (kama ilivyo hapa Tz). Ile namba ina tarakimu chache tu baada ya code number na ikipigwa unaambiwa kuwa haipo!